Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshika nafasi ya Kwanza Kitaifa kwenye Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) uliofanyika nchini kote kuanzia tarehe 08 hadi 09 Septemba, 2021.
Katika Matokeo yaliyotangazwa leo tarehe 30 Oktoba, 2021 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala Mjini) imeongoza Halmashauri nyengine 183 kwa kushika nafasi ya kwanza.
Itakumbukwa kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo kimitihani imegawanywa katika Wilaya Mbili (2) ambazo ni Ilala Mjini na Ilala Vijijini
Katika matokeo hayo, Shule za Ilala Mjini, waliokuwa na idadi ya watahiniwa 13,874 waliofaulu ni 13,699 wakipata ufulu wa 98.52% na kushika nafasi ya kwanza kitaifa
Kwa upande wa Shule za Ilala Vijijini, idadi ya watahiniwa ni 13,846 na waliofaulu ni 13,331 wakipata ufaulu wa 96.28 na wakishika nafasi ya 10 kitaifa.
Hongera kwa Viongozi wa Wilaya ya Ilala wakiongozwa na Mhe. Ludigija, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Kumbilamoto, Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Shauri, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watumishi wote wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Jiji bado tunaongoza
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.