Na. Judith Damas na Amanzi Kimonjo
Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 3 Novemba, 2021 imefanya ziara ya kawaida ya kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2021/ 2022.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Naibu Meya Mhe. Saady Khimji kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza kwa kukagua eneo la ujenzi wa stendi ya kinyerezi ambapo stendi hiyo iliyoambatana na ujenzi wa barabara ya Km 7.5 imekamilika kwa asilimia 81 na kazi inaendelea, maeneo mengine yalitombelewa ni ujenzi wa barabara ya nje katika machinjio ya Vingunguti, Ujenzi wa Mabucha ya Nyama Vingunguti pamoja na Ujenzi wa paa katika soko la Machinga Complex.
Itakumbukwa kuwa baada ya Kuungua kwa Soko kuu la Kariakoo Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa paa katika Soko la Machinga Complex lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya kazi kwa Wafanya biashara kwani maeneo hayo yamejengwa kwa ajili ya wafanya biashara waliotoka katika soko kuu la kariakoo waendelee kufanya biashara zao.
Sambamba na hilo Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Khimji amesema "ujenzi uko vizuri japo kuna marekebisho madogo ambayo inabidi yarekebishwe kwani paa linaonekana kuegemea upande mmoja hivyo inabidi mrekebishe likae sawa kusudi mvua zikianza kunyesha maji yasije yakaharibu bidhaa za wafanyabiashara na wao pia wakashindwa kufanya biashara kwa uhuru."
Aidha, Mhe. Khimji ameeleza kuwa "kupitia ziara yetu ya leo naamini yatafanyika marekebisho ya yale tulio yaona na hivyo kuna umuhimu wakufanya ziara za mara kwa mara ili tuweze kutembelea miradi na tujiridhishe na kushirikiana kwa dhumuni la kufanikisha shughuli za maendeleo pamoja."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.