Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Oktoba 30, 2024 wamefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi mitatu ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Mwanagati - Kwampalange (km 0.5) , pamoja na ujenzi wa Madaraja ya Kasevu na Mzava.
Aidha, ujenzi wa Barabara ya Mwanagati - Kwampalange ukiwa umefikia asilimia 55, hadi kukamilika utagharimu shilingi milioni 681.8 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, huku ujenzi wa madaraja ya Kasevu na Mzava ukiwa umefikia asilimia 56 utagharimu shilingi milioni 522.8 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nyansika Getama akiwa kwenye ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo hivyo nitoe wito kwa watendaji wa Halmashauri kusimamia miradi hii kwa ukaribu na Sisi kama wasimamizi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati na thamani ya Fedha inayotumika inalingana na ubora wa miradi."
Sambamba na hilo, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fungu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kukumbushana kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwaajili ya kutatua changamoto za wananchi ambao wamewaweka wao madarakani.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.