Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 24 Oktoba , 2023 wamefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 (Julai hadi Septemba 2023.)
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi minne (4) ikiwemo ujenzi wa Madarasa ya ghorofa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja, ujenzi wa uwanja wa Mpira Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, ujenzi wa Madarasa 8 na matundu 13 ya Vyoo Shule ya Sekondari Jangwani pamoja na ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Boma.
Aidha, ujenzi wa madarasa 20 ya ghorofa 4 Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja mmoja uliogharimu takribani shilingi Milioni 540 ikiwa kwenye hatua ya Frame work na hadi kukamilika utagharimu shilingi bilioni 1.8, Ujenzi wa Madarasa 8 na Matundu 13 ya Vyoo Shule ya Sekondari Jangwani yenye thamani ya shilingi milioni 199.4 Fedha kutoka kwa wafadhili Barrick Gold Mine ikiwa mchango wao wa kurudisha hisani kwa jamii mbapo Madarasa nane (8) yaliyogharimu shilingi milioni 176 yakiwa yamekamilika huku matundu 13 ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 23.4 yakiwa katika hatua ya ukamilishaji pia ujenzi wa Shule ya Msingi Boma Mpya yenye madarsa sita (6) ya Msingi na Madarasa mawili (2) ya awali, jengo moja (1) la utawala na matundu kumi na sita (16) ya vyoo uliogharimu shilingi milioni 306.9 Fedha kutoka Mradi wa Boost ukiwa umekamilika huku ujenzi wa uwanja wa mpira Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa unaotekelezwa kwa Fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri ukiwa umefikia asilimia 35% ya utekelezaji ambapo hadi kufikia Disemba 31, 2023 mradi huo utakuwa umekamilika na utagharimu shilingi milioni 989.8.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Saady Khimji akifanya majumuisho ya ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo hivyo nitoe wito kwa watendaji wa Halmashauri kusimamia miradi hii kwa ukaribu zaidi na Sisi kama wasimamizi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati na thamani ya Fedha inayotumika inalingana na ubora wa miradi."
Sambamba na hilo Mhe. Khimji ameendelea kusema, "Kamati hufanya ziara hizi kwa lengo la kukagua na kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri zinawafikia walengwa na kufanya kazi kama ambavyo wao wamepitisha kupitia vikao vya Madiwani na kuangalia thamani ya fedha hizo na kazi zinazofanyika hivyo naomba mapungufu yaliyoonekana kwenye miradi hiyo yashughulikiwe kwa wakati na kuweza kufikia hitimisho sahihi kwani tunachohitaji wananchi wote wafikiwe na huduma muhimu na bora kwa wakati kama Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoonesha juhudi zake katika kuwahudumia Wananchi.”
Aidha, Wajumbe wa Kamati wameridhia kuwa endapo kutakua na changamoto wakati wa utekelezaji wa miradi ni vyema changamoto hizo zikawasilishwa sehemu husika mapema na kufanyiwa kazi ili maendeleo ya wananchi yasikwamishwe huku wakiagiza miradi yote ya madarasa ya Boost yatembelewe ili kukagua kama kuna changamoto na zifanyiwe marekebisho kabla madarasa hayo hayajaanza kutumika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.