Na: Shalua Mpanda
Kuna usemi usemao, kama unaitaka mali utaipata shambani. Usemi huu unajidhihirisha kwa mkulima wa zao la Pilipili hoho ndugu Samir Farouk mkazi wa Chanika Jijini Dar es salaam.
Mkulima huyo amebainisha kuwa Kilimo hicho ambacho ukifanya kwa kutumia njia ya Kitalu Nyumba(Green House) kinamuwezesha kupata kipato ambacho kinamuwezesha kujikimu na kuendesha maisha.
''Mimi nina miche mia nane ya hoho hizi nyekundu na njano na kila wiki navuna kilo 80 hadi 100 na kilo moja ni kati ya elfu nne mpaka elfu nne mia tano hivyo nina uhakika wa kupata kati ya laki 6 hadi saba kwa wiki''. Alisema Mkulima huyo
Aidha amesema kilimo cha kutumia "Green house" kina faida kubwa kiafya kwa kuwa hakitumii madawa na hakiathiriwi na wadudu.
Amewataka wakulima na wale wanaopenda kujifunza njia hiyo ya kisasa ya kilimo kufika katika banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nanenane) mkoani Morogoro.
“CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI 2025”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.