Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Jomaary Mrisho Satura ametoa salamu za pongezi kwa Watumishi wake kufuatia ushiriki wao kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, ambapo Mwenge wa Uhuru umepita kwenye miradi (07) na kupokea taarifa ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023.
Akitoa salamu hizo, Mkurugenzi Satura alisema "Ndugu zangu, kwa dhati kabisa ya moyo nawashukuru sana kwa namna ambavyo tumeshiriki kikamilifu kwenye maandalizi na kisha kuukimbiza Mwenge wetu wa Uhuru 2024 katika miradi yetu yote (7) ndani ya Jiji letu la Dar es salaam na kufanikiwa kuvuka salama"
Kwenye salamu zake Mkurugenzi Satura ameeleza hisia zake kwa Watumishi kua "Najisikia fahari kubwa sana kufanya kazi nanyi, naomba 'spirit' hii na 'team work' hii iendelee na kuwa utamaduni wetu wa ufanyaji kazi kila siku na kila mahala"
Aidha, Mkurugenzi Satura alisisitiza kuwa "Nikiwa nafahamu ya kuwa kazi ilikuwa nzito na ngumu na 'probably' mmechoka sana, niwaombe asubuhi hii kwa pamoja tujitahidi kuendelea kuwa na ari na nguvu ili tuweze kuusindikiza Mwenge wetu na kuukabidhi kwa wenzetu wa Wilaya ya Temeke"
Mwisho Mkurugenzi Satura alimalizia kwa kusema "Desturi yangu, kama navyopenda kukemea yasiyofaa kufanywa ndivyo nilivyo mwepesi kupongeza mazuri yanayofanywa. Tufanye mazuri ili kudumisha na kuendeleza mahusiano na upendo wa kweli. Kurugenzi ni Taasisi bila ya ninyi, Mimi siyo lolote wala chochote 'Nawapenda sana nduguJomaary Mrisho Satura ametoa salamu za pongezi kwa Watumishi wake kufuatia ushiriki wao kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, ambapo Mwenge wa Uhuru umepita kwenye miradi (07) na kupokea taarifa ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023. zangu'
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.