Na. Doina Mwambagi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Leo tarehe 25 Januari 2025 ameongoza mamia ya wananchi wa Jiji hilo katika Zoezi la usafi katika eneo la uwanja wa ndege Terminal one kuelekea fukwe za bahari ya Hindi lengo likiwa ni maandalizi ya mapokezi ya ugeni wa maraisi na viongozi wa nchi za Afrika
Akiongea wakati wa Zoezi hilo, Mheshimiwa Chalamila amesema Tanzania imepata heshima kubwa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu zaidi ya 30 wa nchi za Afrika kujadili masuala ya Nishati.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia heshima hii kwa kuwa yeye ndie kinara wa masuala ya nishati Afrika mashariki na Afrika kiujumla.” amesisitiza Chalamila
Aidha, RC Chalamila amesisitiza umuhimu wa kuweka Mkoa katika hali ya usafi nyakati zote za ugeni huo ukiwa katika mkoa wetu na mara baada ya ugeni huo kuondoka tabia ya usafi iwe ni utamaduni wa kila siku kwa kila mtu.
Vilevile, RC Chalamila amesema kutokana na ugeni huo ni mkubwa baadhi ya barabara zitafungwa kwa usalama wa viongozi hao huku akiwataka wananchi kuwa wavumilivu kwa siku chache ambazo ugeni huo utakuwepo nchini.
Mwisho, Mhe. Chalamila amesema mkutano huo unakuja na fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla hivyo amewataka wananchi kutumia vizuri fursa hizo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.