Na: Doina Mwambagi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo amewaagiza wakandarasi wa usafi kuhakikisha wananunua na kutumia vifaa bora vya usafi ili kuboresha hali ya usafi jijini Dar es Salaam.
Ameyasema hayo leo, Februari 15, 2025, mara baada ya zoezi la usafi katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam linalofanyika kila Jumamosi.
"Tuna kazi kubwa ya kufanya Dar es Salaam iwe safi, na tunapaswa kuwa mfano kwa miji mingine. Uwezo tunao, nia tunayo, na lazima tuthibitishe hilo kwa vitendo," alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, amewashukuru wananchi na wadau wa mazingira kwa kushiriki katika zoezi la usafi na kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kusimamia vyema usafi wa jiji na kuhakikisha Dengu beach inakuwa safi na ya kuvutia.
Sambamba na hilo, DC Mpogolo ametoa wito kwa mamlaka husika na wananchi kuhakikisha usafi unadumishwa kila siku, akisisitiza kuwa usafi wa jiji hautakiwi kuwa wa kampeni za mara kwa mara pekee.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, ndugu Elihuruma Mabelya, amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa juhudi zake za kusimamia usafi kila Jumamosi. Amesema kuwa usafi ni utamaduni na tabia inayojengeka, na kwamba Halmashauri ipo tayari kutekeleza agizo la usafi kikamilifu
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.