Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amefungua jengo la Ofisi ya Serikali za Mtaa wa Mwanagati lenye thamani ya shilingi milioni 59 likiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akiongea na Wananchi wa Kata ya Mzinga baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo Mhe. Kumbilamoto amesema “Napenda kutoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kwa ushirikiano wake katika kufanikisha ujenzi wa ofisi hii ambayo itarahisisha huduma kwa Wananchi wa Mtaa wa Mwanagati Kata ya Mzinga pia pamoja na kukamilika kwake bado kuna samani za ndani ambazo hazjakamilika hivyo nipende kuwaahidi kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi tutahakikisha thamani hizo za ofisi zinawafikia kwa wakati ili Wananchi waendelee kupata huduma kwa ukaribu zaidi.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura amesema kuwa uwepo wa Ofisi ya Mtaa wa Mwanagati itasaidia kupumguza kero kwa wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo kwenye Ofisi za Kata ya Mzinga huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la DSM katika kulipa kodi hususani Kodi ya Huduma (Service Levy) pamoja na kukata leseni za biashara lengo likiwa ni kuchochea maendeleo ya Halmashauri ikwani fedha zinazopatikana zinarudi kwenye Kata kufanya maendeleo.
Katika hatua nyingine Ndg. Satura aliweza kutemebelea Kituo cha Polisi Cha Kata ya Mzinga pamoja na Barabara ya Vumbi inayotarajia kuwekwa lami kupitia mradi wa DMDP awamu ya 3 ambapo amewaahidi wananchi wa Kata ya Mzinga kuwa atatenga fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho cha Polisi.
Awali akiongea Katika Hafla hiyo Meneja wa Kanda namba 6 (Kivule) Bi. Salma Said amewataka Wananchi wa Kata ya Mzinga kufika ofisi za Kanda Kivule kupata huduma zote za msingi kwani huduma zimesogezwa karibu zaidi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.