Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila leo Septemba 22, 2023 amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mchikichini kinachojengwa kwa shilingi Bilioni 5.2 Fedha kutoka Serikali Kuu na Mapato ya Ndani ya Halmashauri pamoja na Ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti wenye thamani ya shilingi bilioni 5 Fedha kutoka Pochi la Mama, Fedha kutoka mradi wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Program) na Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Mativila amemuelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha kuwa endapo Mkandarasi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mchikichini anashindwa kuendana na kasi ya muda aliopewa ni vyema kutafuta Mkandarasi mwingine kwani lengo kubwa ni Kituo cha Afya kukamilika kwa wakati na Wananchi kupata huduma kwa wakati na ukaribu zaidi.
Sambamba na hilo Mhandisi Mativila amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya pamoja na ujenzi wa Shule ili kuchochea uchumi na Huduma za Jamii kuwafikia Wananchi kwa ukaribu zaidi.
"Nimekuja kutembelea na kujionea ujenzi wa miradi hii ya Maendeleo, napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kuchochea Maendeleo Kwani fedha za pochi la mama zimeonyesha juhudi kubwa katika kukamilisha mradi huu wa Shule ya Sekondari Liwiti kwani huduma hizi muhimu zitasaidia kukuza sekta ya Elimu na Afya nchi hivyo niwaombe miradi hii itekelezwe kwa ubora ili iweze kudumu kwa muda mrefu." alisema Mhandisi Mativila.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomary Satura amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la DSM huku akimuahidi kuendelea kusimamia vizuri fedha za Serikali zinazotumika katika utekelezaji wa miradi pamoja na kutekeleza yale yote aliyowaelekeza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.