Na: Doina Mwambagi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inahitaji wawekezaji wanaojibu na kutatua changamoto za Wananchi.
Ameyasema hayo leo Januari 23, 2025 kwenye hafla ya uzinduzi wa mashirikiano baina ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Azam Marine iliyofanyika eneo la Magogoni Jijini Dar es Salaam.
"Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya ujenzi kwa kusikia kilio cha wananchi wa Magogoni na Kigamboni kwa kuruhusu Azam Marine kuwekeza katika vivuko vyake vya taxi ya baharini (Sea Taxi) ili waweze kutatua tatizo la foleni na msongamano wa wananchi wa pande hizi mbili". Alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya vivuko kujinasua kiuchumi kwa kuwahi maeneo mbalimbali ya biashara na kazi huku akiwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika fukwe za bahari ya Hindi.
Eneo la Kigamboni limekuwa na changamoto ya muda mrefu ya msongamano wa watu hasa nyakati za asubuhi na jioni kufuatia baadhi ya vivuko vyake ikiwemo Mv.Kigamboni na Mv.Magogoni kuwa katika matengenezo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.