Na: Shalua Mpanda
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu ametumia Kongamano la Wajasiriamali kutoa maelekezo kwa maafisa Maendeleo ya Jamii kutenda haki katika kutoa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Zungu amesema lengo la mikopo hiyo ni kuwakwamua wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi hivyo Maafisa hao hawana budi kutenda haki na kuhakikisha wale wote wenye vigezo wanapata mikopo hiyo.
"Kuna baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii hawatendi haki kwenye kutoa mikopo hiyo na hilo limekuwa likiwaletea changamoto sana wananchi,hivyo niwatake maafisa Maendeleo ya Jamii mtende haki kwenye hili". Alisisitiza Mhe. Zungu
Awali akitoa maelezo kuhusu mikopo hiyo ya asilimia 10 ambayo hutolewa kwa makundi hayo matatu, Mkurugenzi wa Jiji la DSM Elihuruma Mabelya amesema Jiji hilo limetenga kiasi Shilingi Bilioni 14 kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali kutoka Kata ote 36 za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.