• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kilimo

Utangulizi

Kilimo ni Sekta muhimu kwa maisha na uchumi wa wakazi wa Mjini na pembezoni mwa Mji.

Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa Mikoa ambayo Kilimo huchangia katika kuongeza kipato kwa wakazi, upatikanaji wa chakula (lishe bora) na hifadhi ya mazingira. Takribani asilimia thelathini (30%) ya mazao ya kilimo yanayotumiwa na wakazi wa Jiji huzalishwa katika maeneo mbalimbali katikati na pembezoni mwa Jiji. Mboga za majani na matunda ni mazao muhimu yanayozalishwa kutokana na kuwa karibu na soko (walaji) na bei nzuri. Mboga zinazozalishwa ni mchicha, matembele, chainizi kabichi, bamia, kisamvu, sukuma wiki, bilinganya, uyoga, mnavu, kisamvu na maboga. Matunda ni pamoja na makakara, matango, papai, nanasi, matikiti maji, na machungwa.

Fursa zilizoko katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa Sekta ya Kilimo:

Mkoa una fursa nyingi katika kilimo kutokana na kuwa karibu na soko kubwa (walaji), makampuni ya usindikaji na miundombinu mizuri ya usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi. Mkoa una makampuni makubwa na madogo ya usindikaji wa mazao ya kilimo kama vile matunda, nafaka, na viwanda vya nguo.

Aidha maduka makubwa ya kisasa (shopping malls) yanayoendelea kuongezeka yamekuwa chanzo kingine cha soko la mazao ya kilimo. Mwingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam ni chanzo kingine cha soko la bidhaa mbalimbali za kilimo. Tabia ya ulaji (feeding habit) za watu wa mataifa mbalimbali hutoa wigo mpana kwa wazalishaji kupanua wigo wa mazao kulingana na mahitaji halisi. Katika kupanua wigo wa mazao ya kilimo, Mkoa umeanzisha zao la mchicha nafaka ambao kwa mujibu wa wataalam wa lishe umeonesha kuwa na virutubisho muhimu kwa afya ya mlaji. Mchicha huu huzalishwa kwa wingi kupitia vikundi vya wakulima wa manispaa ya Kinondoni.
 
Vilevile kadri kipato kinavyoongezeka ndivyo jamii inavyojali ubora wa chakula (food quality) kuliko wingi (food quantity). Takwimu zinaonesha kuwa kaya za jijini Dar es Salaam zina kiwango kidogo cha umaskini wa mahitaji ya msingi ukilinganisha na kaya zinazoishi katika miji mingine na maeneo ya vijijini. Hii ni fursa kwa wazalishaji, wataalam wa ugani, wawekezaji na wadau mbalimbali wa kilimo kuongeza thamani katika bidhaa za kilimo na kuzingatia ubora katika uzalishaji, hususani matumizi ya kilimo hai (organic agriculture) ili kuchangamkia fursa hii inayoongezeka kwa kasi kutokana na kukua kwa kipato na uelewa wa wakazi wa Dar es Salaam.

Mazao kama vile korosho, muhogo na viazi huzalishwa kwa wingi katika Manispaa ya Temeke na Ilala. Usindikaji wa unga wa muhogo na korosho hufanywa kupitia vikundi vilivyopo katika Manispaa za Ilala na Temeke. Uwepo wa Bandari ya Dar es Salaam, barabara zinazokwenda mataifa jirani, Mamlaka za Serikali kama vile Wizara mbalimbali za Kisekta ni fursa ambazo zinaweza kutumiwa na wazalishaji, wasindikaji na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo katika kuzalisha, kusindika na kusafirisha bidhaa za kilimo nje ya nchi na kujipatia fedha za kigeni kwa ustawi wa taifa letu. Aidha uwepo wa taasisi nyingi za fedha, taasisi za utafiti, NGOs zinazojihusisha na kilimo vyote kwa ujumla vinaweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa kilimo mjini (urban agriculture).
 

Udongo na hali ya mwinuko:

Mkoa umetawaliwa kwa kiasi kikubwa na udongo wa kichanga kwa takribani kanda zote za kilimo. Kuna ukanda wa juu ambao umezungukwa na miinuko. Maeneo haya ni yale ya Magharibi na Kaskazini mwa Jiji. Ukanda wa chini umeundwa na mabonde ya Msimbazi, Jangwani, Mtoni, Afrikana, Kimbiji, Kitunda na maeneo ya Ununio na Mbweni .

Eneo linalofaa kwa kilimo na ufugaji ni hekta 107,500, ambapo Manispaa ya Temeke ni hekta 55,000, Kinondoni hekta 37,000 na Ilala hekta 15,000. Hadi sasa eneo linalotumika kwa kilimo ni Ha.32, 972 sawa na asilimia 31 ya eneo lote. Changamoto inayoikumba Sekta ya Kilimo katika mkoa wa Dar es Salaam ni kupungua kwa ardhi ya kilimo kutokana na mashamba kutwaliwa kwa ajili ya viwanja vya makazi na uwekezaji mbalimbali.


Masoko makuu:

Mkoa una masoko makuu ambapo bidhaa mbalimbali za kilimo hupatikana. Masoko hayo yanapatikana katika Halmashuri tatu za Manispaa (Ilala, Kinondoni, Temeke Ubungo na Kigamboni).

Ilala

  • Kariakoo : Limesheheni bidhaa mchanganyiko ikiwa ni pamoja na maduka ya pembejeo
  • Buguruni : Bidhaa zinazopatikana kwa wingi ni bidhaa za kilimo kama vile nafaka mbalimbali, mhogo, viazi na matunda.
  • Kigogo Sambusa : Ni maarufu kwa mboga za majani.
  • Ilala : Bidhaa kuu zinazopatikana ni matunda (fresh fruits) na mboga.

Kinondoni

  • Tandale : Ni maarufu kwa nafaka, matunda na maharage.
  • Manzese : Ni maarufu kwa unga wa mahindi.
  • Mabibo : Bidhaa kuu ni ndizi, viazi mviringo na matunda.
  • Mwananyamala : Ni maarufu kwa nafaka na bidhaa mchanganyiko.
  • Makumbusho : bidhaa zinazopatikana kwa wingi ni viazi mviringo na bidhaa mchanganyiko.

Temeke

  • Tandika : Maarufu kwa nafaka,
  • Temeke Sterio : Maarufu kwa matunda, viazi vitamu na mviringo, nyanya na bidhaa mchanganyiko.
  • Vetenari : Ni maarufu kwa ndizi mbivu, parachichi na matunda mchanganyiko.
  • Mbagala Rangi Tatu : Bidha kuu ni nafaka, unga wa mahindi, viazi mviringo na mbogamboga.
  • Mtoni Mtongani : Bidha zinazopatikana kwa wingi ni nafaka, unga wa mahindi, viazi mviringo na mbogamboga.

Changamoto:

Changamoto dhidi ya kilimo ni kupanuka kwa kasi kwa Jiji hivyo maeneo mengi ya kilimo kufanywa makazi ya watu na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii. Hii ni fursa pia kwa uzalishaji wa mazao yenye thamani (high value crops) na matumizi ya teknolojia zinazohitaji eneo dogo la ardhi kama vile "green houses" ili kufanikisha kilimo-biashara mjini. Aidha kumekuwa na uharibifu mkubwa wa bidhaa sokoni (post harvest loss) kutokana na miundombinu mibovu ya masoko na ukosefu wa maghala ya kisasa. Hii ni fursa kwa wawekezaji kuanza kufikiria kuwekeza katika miundombinu kama vile "cold rooms" na maghala ya kisasa (silos) ili kupunguza uharibifu ambao umekuwa ukiathiri hali ya usalama wa chakula katika Jiji la Dar es Salaam.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.