Unaweza kusema ni kama ndoto kwa wakazi wa kata ya Bonyokwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam mara baada ya kushuhudia ujenzi wa shule ya kisasa ya kidato cha tano na cha sita ndani ya Halmashauri hii ukishika kasi.
Ujenzi huo wa shule ya ghorofa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.7 unaojumuisha madarasa 53 na matundu ya vyoo 45 ambao mpaka sasa umefikia asilimia 52 unaelezwa na wakazi wa Kata hiyo kuwa mara baada ya kukamilika kwake utasaidia kupunguza adha ya watoto wao kufuata elimu mbali na eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio chao cha muda mrefu kuhusu kupatikana kwa shule ya aina hiyo katika kata yao.
'Hatuna la kusema kwa kweli huu ujenzi wa shule hii ulikuwa unatuumiza vichwa kuwa lini utakamilika, lakini sasa hivi ni kama tunaona ndoto tunavyoona mradi huu unavyoenda kwa kasi, tunamshukuru sana mama (Rais Dkt. Samia) ". Alisema Bi. Nasra Ayoub.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema ujenzi wa shule hiyo ya kisasa ambayo itakuwa na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwemo lifti umetekelezwa kwa makusanyo ya fedha za ndani za Halmashauri.
Mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi kampuni ya Platnum Construction unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ambapo kwa sasa umefikia hatua ya umaliziaji(finishing).
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.