SEKTA YA MIFUGO.
Sekta ya Mifugo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu katika uchumi wa watu binafsi, Kaya na Taifa. Ufugaji upo wa mifugo ya aina mbalimbali wakiwemo wanyama wakubwa na wadogo, kwa ajili ya chakula, biashara, wanyama kazi na wanyama rafiki (pets).
HUDUMA ZA MIFUGO.
Miongoni mwa huduma za Mifugo zinazotolewaa na Maafisa Ugani ni pamoja na kuhasi, uhamilishaji,kukata pembe,kukata kwato, kukata meno(Nguruwe), kukata midomo (Kuku), kutoa huduma ya chanjo, kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya Mifugo, ukaguzi wa Mifugo na Mazao yake, kutoa vibali mbalimbali kwa mujibu wa Sheria( Vibali vya kusafirisha mifugo na mazao yake na vibali vya kupatiwa chanjo ya Kichaa cha Mbwa kwa Binadamu.) na kutoa ushauri wa kitaalam kwa Wafugaji.
AINA NA IDADI YA MIFUGO KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM.
AINA
|
KISASA
|
ASILI
|
JUMLA
|
Ng’ombe
|
37,993
|
10,451
|
48,444
|
Mbuzi
|
1,185
|
21,756
|
22,941
|
Kondoo
|
-
|
5,698
|
5,698
|
Nguruwe
|
43,022
|
-
|
43,022
|
Kuku
|
6,135,371
|
708,263
|
6,843,634
|
Mifugo mingine iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni bata, kanga, kwale, sungura, simbilisi, mbwa, punda, farasi, ngamia na paka.
MIUNDOMBINU ILIYOPO NA INAYOFANYA KAZI NI:
Maduka/ Maeneo ambayo pembejeo za mifugo (vyakula vya mifugo, madawa, chanjo) pamoja na vituo vya huduma kwa mifugo
Viwanda vya usindikaji wa mazao ya Mifugo ambavyo ni viwanda vya Maziwa, viwanda vya ngozi, viwanda vya nyama na viwanda vya vyakula vya Mifugo.
Miundombinu mingine ni Mnada wa Upili wa Mifugo (Secondary Livestock Market), majosho, malambo, mabirika, vibanio, mabanda ya ngozi, machinjio, machinjio (slabs) (kwa ajili ya ng’ombe, nguruwe, kuku na ndege wengine).
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.