Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inamiliki kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1999 kwa lengo la kuondoa msongamano wa mabasi yaliyokuwepo katika vituo vidogo vidogo vilivyokuwepo katikati ya Jiji. Tangu kuanzishwa kwake Kituo cha mabasi cha Ubungo kimekuwa kikitoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi pamoja na kutoa huduma, kituo hiki pia ni chanzo kikuu cha mapato cha Halmashauri ya Jiji.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga fedha za ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya DART ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo na kupunguza msongamano wa magari katika eneo la Ubungo.
Katika kutekeleza mradi huu, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imekamilisha maandalizi ya uandaaji wa taarifa mbalimbali kuhusu mradi kama:
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pia imefanikiwa kupangiwa fedha za Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya kimkakati kiasi cha shilingi 50,689,000,000.00 ili kuweza kutekeleza ujenzi wa miundombinu wa Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis.
Michoro ya mwonekano wa Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.