• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Utalii

UTALII KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana katika   uchumi wa Tanzania. Unapatikana katika pwani ya Bahari ya Hindi na una Bandari kubwa katika Afrika mashariki unaoufanya mkoa huu kuwa mashuhuri sana kiuchumu. Una miundombinu ya uhakika ambayo ni barabara nzuri za lami, hoteli zenye hadhi ya kuanzia nyota 1 hadi  5 na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ujulikanao kama (Mwalimu Nyerere International Air Port). Uwepo wa Bandari kubwa na ya kisasa unaufanya Mkoa uweze  kufikika kirahisi kwa kupitia Baharini na Nchikavu kutoka katika kila pembe ya Dunia na kuwa kiungo muhimu katika Sekta ya Utalii.

Mkoa wa Dar es Salaam hauko nyuma katika Sekta ya utalii. Mkoa huu una vivutio vingi ambavyo ni muhimu katika kuvutia watalii. Vivutio vya asili vilivyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Bahari yenye fukwe nzuri, Misitu ya Mikoko na Miyombo, Visiwa, Matumbawe na hifadhi ya wanyama Dar es Salaam zoo.

Dar es Salaam ina uoto wa asili wa aina mbili ambao ni Misitu ya Mikoko yenye ukubwa wa hekta 2760 na Miyombo yenye ukubwa wa hekta 1380.  Misitu ya Mikoko inapatikana katika mwabao wa Bahari ya Hindi na Misitu ya Miyombo inapakika katika maeneo ya uwanda wa juu. Misitu hii imehifadhiwa kwa ajili ya makazi na mazalia ya viumbe wa baharini na nchi kavu na ni kivutio kizuri cha utalii katika mkoa wetu.

Uwepo wa Bahari ya Hindi katika Mkoa huu ni kivutio kizuri sana cha utalii kwa kutoa muonekano unaovutia na kuleta upepo mzuri. Bahari inaweza kutumika kwa kufanya mashindano ya kuendesha boti pamoja na kuogelea. Bahari vilevile ni hifadhi ya samaki wengi wanaovutia. Ufukwe mzuri wa Koko wenye eneo kubwa la kupumzika ni kivutio kizuri cha utalii kwa wenyeji na wageni

Mkoa vilevile una visiwa vikubwa vitatu vilivyo umbali kidogo kutoka katika ufukwe wa Bahari. Visiwa hivyo ni  Mbudya, Bongoyo na Pangavini. Visiwa hivi vina misitu mikubwa ya asili inayopendesha mazingira na ni makazi ya viumbe wa nchi kavu kama vile ndege na nyoka. Vimezungukwa na miamba ya matumbawe (coral reefs) ya rangi mbalimbali na ni mazalia ya samaki.

Mkoa huu una vivutio vingi vya kale ambavyo ni mabaki ya tokea Utawala wa Mwarabu, Mjerumani na Muingereza pamoja na mabaki ya zana na watu wa kale. Mabaki haya yanaonekana kama alama zilizopo ardhini na kwenye majengo.

  • Makumbusho ya Taifa yanayoonesha mabaki ya mafuvu ya binadamu wa kale pamoja na nyayo kutoka katika mapango maarufu ya Olduvai, Hifadhi ya zana za kale za uhunzi pamoja na picha za asili ya makabila mbalimabali.
  • Kijiji cha Makumbusho ni kivutio kizuri cha utalii kinachoonesha tamaduni za makabila yasipungua 100 ya Tanzania. Kinazo nyumba za asili zilizojengwa kwa tope na kuezekwa kwa nyasi na tope. Vivevile kina michoro ya asili, mikeka iliyosukwa kwa mikono na ngoma za asili zinazovutia kucheza.
  • Kunduchi Beach yenye mabwawa makubwa ya kuogelea pamoja na Uwanda mkubwa wa Bahari unaotumika kwa michezo ya kukimbizana kwa pikipiki za majini ni kivutio kikubwa cha utalii katika Mkoa wetu. Katika hoteli hii kuna maeneo yaliyotengenezwa kwa ajili ya michezo ya watoto na migahawa ya vyakula ambavyo hutia hamasa kutembelea maeneo haya.
  • Vivutio vingine mbalimbali vinavyobeba historia ya ukoloni kuanzia Utawala wa Mwarabu hadi Muingereza ni uwepo wa nyumba za ibada kama vile Msikiti wa Mtoro na Nyamwezi iliyopo Kariakoo, Kanisa  (St. Joseph’s, The White Father’s Mission House), 
  • Ikulu Ofisi kuu ya Utawala wa nchi hii yenye usanifu wa kale iliyopambwa na ndege wazuri wasiopatikana eneo lolote Duniani kivutio kizuri cha utalii katika mkoa wetu.
  • Vilevile Mkoa unatambulika kwa kuwa na hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo zinatoa uhakika wa malazi salama kwa watalii.

Ushirikiano na Miji mingine ya Utalii Duniani ni jambo muhimu sana, tunaweza kuibadilisha Dar es Salaam kuwa Jiji kuu la Utalii Duniani na kuliongezea Taifa kipato. Si hivyo tu bali uchumi wa watu utabadilika na kupunguza umasikini. Kwa kuzingatia kwamba Serikali yetu inasisitiza mabadiliko katika kuboresha uchumi wa viwanda ili kuondoa umasikini na kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

 

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.