Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limefanya kikao cha kupitia na kupitisha sheria ndogo za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Machi 6, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou, Jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kufanyia marekebesho madogo ya sheria za awali katika maeneo ya ushuru wa Masoko, tozo za fremu za maduka pamoja na ada ya ulinzi shirikishi.
Akiongea katika kikao hichokikao Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Ojambi Massaburi ambaye aliongoza Kikao kwa Niaba ya Mstahiki Meya, amesema kanuni inaeleza vizuri kwani lengo sisi ni kupitia sheria hizi na kuzifanyia marekebisho lengo likiwa ni kutomuumiza mwananchi yoyote wala kumpendelea mtu yoyote kwani sheria hizi zinadumu kwa muda mrefu hivyo tuzifate na kuzisimamia.
Wakijadili marekebishio ya sheria hizo kabla ya kuzipitisha baraza la Madiwani limeridhia kuwa kwa upande wa ushuru wa masoko tozo zitengwe kulingana na eneo Soko lilipo kwani masoko ya pembezoni mwa mji hawawezi kukidhi mahitaji ya kulipia fremu za Masoko kama Masoko ya mjini.
Adhia Vikundi vya Ulinzi Shirikishi kuanzia ngazi ya Mtaa ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ndiye msimamizi wa zoezi hilo na katika ngazi ya Kata Mtendaji wa Kata ndiye msimamizi wa Kata husika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.