Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 02 Machi, 2022 limefanya kikao chake cha kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2022.
Kikao hicho kilichoongozwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam kiliweza kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Fedha na Utawala, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Kamati ya mipango Miji na Mazingira pamoja na Kamati ya Kuthibiti Ukimwi lengo kwa kipindi cha Oktoba Mpaka Disemba 2022 likiwa ni kujiridhisha juu ya utendaji kazi wa kamati hizo.
Sambamba na hilo Kamati ya kuthibiti Ukimwi na Huduma za jamii wameweza kuandaa mafunzo kwaajili ya kutoa elimu ya Afya kwa wananchi na pia katika mafunzo hayo kutakua na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo EBOLA.
Aidha baraza limeweza kujadili mambo mengineyo ikiwemo kero ya usafi kwa wakazi wa Kinyamwezi kwani wakazi hao wanapata shida mara kwa mara kwa kuwa wapo karibu na eneo la Dampo ambapo Dampo hilo hulipuka mara kwa mara hivyo baraza limeridhia kuhakikisha milioni 300 zilizotengwa ziweze kutumika kwa uharaka zaidi ili kuokoa hali ya usafi kwa wakazi wa Kinyamwezi.
Akitoa maelekezo kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Bi. Elly Makala amesema ”Mapambano dhidi ya rushwa siyo ya Taasisi na Serikali peke yake bali wote tunahusika katika kupambana na rushwa, katika kutekeleza hilo TAKUKURU imekuja na mpango mpya unaoitwaTAKUKURU RAFIKI yenye lengo la kuibua kero zilizopo kwenye jamii na kuweza kuzitafutia ufumbuzi ambapo programu hiyo imeshaanza, na katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kushirikisha jamii katika kuibua na kusimamia miradi hiyo kwani lengo la Serikali ni kuinua Ustawi wa Wananchi.”
Aidha Baraza liliridhia na kupitisha taarifa hizo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.