Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 24 Mei, 2023 limefanya Kikao chake cha Kawaida cha kupitisha na kujadili Taarifa ya Utendaji Kazi kwa kipindi cha robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023.
Aidha, Baraza liliweza kupitia Taarifa za Utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Fedha na Utawala, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira pamoja na Kamati ya Kuthibiti UKIMWI kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2023 lengo likiwa ni kujiridhisha juu ya utendaji kazi wa kamati hizo.
Sambamba na hilo Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii iliweza kuwasilisha taarifa ya mradi wa Boost unaotekelezwa katika Shule za Msingi ambapo Kamati iliweza kuwasilisha mgawanyo wa Madarasa katika Shule za Msingi na Awali kwani shilingi bilioni 2.1 imepokelewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwaajili ya utekelezaji wa miradi hivyo Kamati hiyo imesoma taarifa hiyo kwenye baraza la Madiwani lengo likiwa ni kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa kwa ukaribu zaidi na zinatumika kama ilivyo tarajiwa.
Aidha, Baraza limeweza kujadili mambo mengineyo ikiwemo kero ya usafi kwa wakazi wa Mnyamani kwani inaonekana kuna viwanda vimeunganisha maji ya viwandani na bomba la mvua ambapo maji ni kero kwa Wananchi wa Mnyamani lakini pia ni uchafuzi wa mazingira hivyo wajumbe wa Baraza wameridhia viwanda hivyo vishughulikiwe mapema kabla hatua za Kisheria hazijachukuliwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.