Na: Shalua Mpanda
Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amesema Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 170 kutengeneza miundombinu ya kutibu majitaka katika mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Aweso ameyasema hayo wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi huo baina ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kupitia kampuni ya MC Colon Global Corporation.
Amesema kiasi hicho cha fedha kitatumika kutengeneza miundombinu hiyo katika wilaya ya Kinondoni na Ilala ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya majitaka katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa huu.
"Utekelezaji wa Mradi huu utachukua muda wa miezi 36 na kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma wa maji safi na usafi wa Mazingira kutoka asilimia 45 za sasa hadi 65''. Alisema Waziri Aweso.
Awali akitoa maelezo ya Mradi huo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire amesema mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati ya Serikali yenye lengo la kutunza mazingira.
Utiaji huo wa saini umeshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Balozi wa Korea Kusini Nchini Bi. EunJoo Ahn, Wastahiki Meya wa Manispaa pamoja Wakurugenzi wa Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.