• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

DC Ludigija afungua mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Wilaya kwa mwaka 2022

Posted on: July 1st, 2022

Na: Hashim Jumbe

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija, leo tarehe 01 Julai, 2022 amefungua rasmi mashindano ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi Tanzania, maarufu kama  UMITASHUMTA kwa ngazi ya Wilaya ya Ilala.


Mashindano hayo yanayofanyika kwa siku 3 kwenye viwanja vya Shule ya Kebby vilivyopo Pugu Kinyamwezi, yalianzia kwa kushindanishwa timu za madarasa, shule, kata na hatimaye kufikia kutengeneza timu za Klasta, ambazo leo zimeanza kushindanishwa ili kutengeneza timu itakayowakilisha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenye ngazi ya UMITASHUMTA Mkoa.


"Mheshimiwa Mgeni rasmi, mbele yako ni wanamichezo 480 pamoja na walimu wao kutoka Klasta za Chanika, Ukonga, Kimanga na Gerezani ambao leo wanaanza rasmi Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya wilaya. Mashindano haya yanashirikisha michezo ya wavu, soka, riadha, netboli, mpira wa mikono, ngoma na kwaya" alisema Bi. Asha Mapunda ambaye ni Afisa Elimu Michezo wa Idara ya Elimu Msingi Jiji la Dar es Salaam


Naye Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Tenga akiongea wakati akimkaribisha Mgeni rasmi alisema "Wilaya yetu imekuwa ikifanya vyema sana katika mashindano ya UMITASHUMTA na hata taaluma. Mwaka 2021 tuliweza kupata nafasi ya kwanza kitaifa kwa upande wa ngoma na nafasi ya 8 upande wa kwaya, pia tuliweza kutoa idadi kubwa ya wachezaji  72 kati ya 100 ambao ni sawa na 70% kwa  waliounda  timu ya  Mkoa wa Dar es salaam"


Mashindano ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2022 yanabeba kauli mbiu isemayo  “TAKWIMU SAHIHI NI MSINGI WA MIPANGO BORA YA TAIFA” SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI KWA MAENDELEO YETU.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati akifungua mashindano hayo aliwakumbusha wanafunzi hao lengo la wao kuwepo hapo "lengo la mashindano haya ni kushindanisha wanafunzi katika  michezo mbalimbali ili kuibua vipaji vya vijana watakaounda timu bora ya wilaya na baadaye kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Dar es salaam, niwaase kucheza kwa juhudi ili tupate timu itakayokwenda kushindana ngazi ya Mkoa na kuibuka washindi, siku zote Ilala sisi ni washindi" Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija


Ikumbukwe kuwa timu ya Wilaya ya Ilala ndiyo inayoshikilia ubingwa wa UMITASHUMTA kwa ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka minne (4) mfululizo, hivyo kuwa na nafasi nzuri kwa mwaka huu kushinda kwa mara ya tano (5) mfululizo.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.