Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam imesema imeridhishwa na matumizi ya fedha na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ile inayotekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba leo tarehe 04 Januari, 2020 jijini Dar es Salaam akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuelekea Maadhimisho ya Miaka 43 ya CCM tangu kuasisiwa kwake na amesema miradi hiyo ikikamilika italeta tija kwa wananchi.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kuingia eneo la dampo la Pugu Kinyamwezi ikiwemo ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege yenye urefu wa km. 1, ujenzi wa ukuta kuzunguka dampo, ujenzi wa mifereji na makaravati ya maji ya mvua na uwekaji wa mtandao wa maji safi ya bomba kutoka mradi wa GOPU eneo la Dunda, Mwakanga Kigogo
Wajumbe hao pia walipata fursa ya kutembelea Mradi wa Kimkakati wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Mbezi Luis unaokadiriwa kugharimu kiasi cha jumla ya Shilingi 50,947,589,580.20 bila kodi ya zuio "VAT Exclusive" fedha kutoka Serikali Kuu na ambao hadi sasa umeshatekelezwa kwa asilimia 57.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.