Na: Shalua Mpanda
Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) upande wa wanawake kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeendeleza ubabe kwa timu zinazoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA mkoani Tanga kwa kuifumua timu kutoka Halmashauri ya manispaa Kahama kwa seti 2-1.
Mchezo huo uliokuwa mgumu kwa timu zote mbili ulishuhudia timu ya Kahama ikiongoza kwa pointi 25-17 katika seti ya kwanza, Dar City wakashinda seti ya pili kwa pointi 25-17 na seti ya tatu kwa pointi 15-8.
Timu ya Dar City imeendelea kutoa dozi mfululizo katika mashindano hayo na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua zinazofuata katika Mashindano haya.
Mashindano haya ni maalum kwa Halmashauri zote nchini ambapo hushiriki michezo mbalimbali ili kuwakutanisha watumishi wa Halmshauri hizo kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kudumisha mahusiano ya kikazi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.