• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

DC Ilala azindua madarasa 310 yaliyojengwa kwa Fedha ya Pochi la Mama

Posted on: January 6th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija, leo tarahe 06 Januari, 2023 amezindua Madarasa 10 yaliyokamilika katika Shule ya Sekondari Nguvu Mpya iliyopo Chanika Jijini Dar es Salaam, madarasa hayo ni miongoni mwa madarasa 310 yaliyojengwa kwa fedha ya Pochi la Mama, ambapo shule hiyo ilipokea kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo 10, ofisi ya Walimu na ununuzi wa viti na meza.

Katika uzinduzi huo Mh. Ludigija amemshukuru Mheshimiwa  Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuipatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kiasi cha Shilingi Bilion 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 310 "Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea kiasi cha shilingi bil 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 310, kuanzia Jumatatu ambapo shule zinaenda kufunguliwa hakuna mtoto kwenye Halmashauri yetu ya Jiji la Dar es Salaam atakayeshindwa kuingia shuleni kwa sababu ya madarasa, Mama amefungua pochi na pochi lenyewe ndilo hili linaonekana” Amesema Mhe. Ludigija.

Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru amesema Halmashauri imejipanga kwa kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 700 kwa ajili ya kufidia idadi ya madawati yaliyopungua. Vilevile  itatumia mapato yake ya ndani  kwa kujenga  matundu ya vyoo kulingana na idadi ya ongezeko la wanafunzi kwa shule zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Mhandisi Mafuru amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya wa Ilala kuwa kila mtoto atakaa kwenye kiti na meza yake.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe Jerry Silaa, ametoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani fedha za Pochi la Mama zimesaidia wananchi hasa wanafunzi wa Jimbo lake kwa ujenzi madarasa ya shule zilizopo Jimbo la Ukonga, ambapo Jimbo hilo peke yake limepokea kiasi Shilingi billion 4.6. “Nitoe pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais kwani Jimbo la Ukonga limependelewa tumepokea kiasi cha shilingi billion 4.6 na siyo kwamba limependelewa ni kwa sababu lina idadi kubwa ya watu.” Amesema Mhe. Silaa

Akihitimisha  Mkuu wa Shule ya Sekondari Nguvu Mpya, Bwana.Daniel Mwakyambiki amewataka walimu kuwa waadilifu na waaminifu wanapopokea fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kufuata sheria na taratibu.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.