• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

DC Mpogolo alipongeza Jiji la DSM kwa kuboresha Sekta ya Afya

Posted on: June 28th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Pongezi hizo amezitoa leo Juni 28, 2024 wakati wa Hafla ya ugawaji vifaa tiba kwa Idara ya Afya iliyofanyika katika ukumbi wa Arnatoglou Jijini humo.

Akikabidhi vifaa hivyo Mhe Mpogolo amesema “Napenda kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ukusanyaji wa mapato zaidi ya bilioni 100 ambapo wameweza kuvuka lengo la kukusanya bilioni 89 kwani kupitia fedha hizi wameweza kununua vifaa tiba vya shiingi Bilioni 1.6 huku zaidi ya milioni miatatu zikitumika kununua vifaa vya TEHAMA na Milioni 11 zikitumika kukata bima za iCHF kwa watoa huduma za afya ngazi ya Jamii hivyo kutokana na vifaa hivi huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na hii inaonesha jinsi gani Jiji la Dar es Salaam linatimiza adhma ya Mheshimiwa Rais WaJamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na zinawafikia wananchi kwa wakati.”

Sambamba na hilo, Mhe.Mpogolo aliweza kukabidhi vyeti vya mafunzo kwa timu za usimamizi vituoni (HMT’S 164) pamoja na bima za afya 277 kwa watoa huduma ngazi ya jamii huku akiwataka watoa huduma za jamii ngazi ya afya kuwa waadilifu kwa kuhakikisha wanazingatia utoaji wa huduma bora kwa wananchi pamoja na kutoa wito kwa viongozi waliopatiwa vyeti vya mafunzo kuhakikisha wanajali wananchi wanaowahudumia bila kusahau kubainisha changamoto za afya zilizopo ngazi ya jamii ili zipatiwe ufumbuzi.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto  ameeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam limepata bahati ya kupata fedha nyingi kutoka Serikali Kuu ambazo zinatumika kwenye Miradi ya Afya , Elimu na kuboresha miundombinu ya afya hivyo kutokana na ukusanyaji mkubwa wa mapato Jiji la Dar es Salaam limeweza kununua vifaa tiba ili kuhakikisha huduma za afya katika Jiji hilo zinaimarika kwa kasi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya huku alieleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani inaenda kutekeleza ujenzi wa hospitali kubwa tatu zitakazoenda kupunguza changamoto ya msongamano wa wagonjwa pamoja na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati.

Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya, Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Zaituni Hamza ameeleza kuwa “Katika kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa jamii, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Afya ilipanga kununua vifaa tiba mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 vya jumla ya shilingi bilioni 1.6 ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na Serikali kuu ambapo leo tumeweza kukabidhiwa Ultra Sound 15 pamoja na vifaa vya TEHAMA ambavyo vinaenda kuleta mabadiliko katika sekta afya kwenye Jiji letu hivyo tunaahidi kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili wananchi waweze kupata huduma bora kwa wakati.”




Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.