Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Agosti ,2023 amefanya ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Pugu ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafikia wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
Katika ziara hiyo Mhe. Mpogolo aliambatana na Wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wengine kutoka Taasisi wezeshi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu zaidi ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) pamoja na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA).
Akiwa katika kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Pugu Mhe. Mpogolo amesema amebaini kero kubwa kutoka kwa wananchi wa Pugu Kinyamwezi ni kukosekana kwa Shule ya Msingi ya Karibu, Barabara zisizopitika pamoja na uvamizi wa ardhi.
Hata hivyo Mhe. Mpogolo amewataka Viongozi wa Serikali za Mtaa wa Pugu-Kinyamwezi kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la ardhi hususani maeneo yaliyoachwa wazi kwani maeneo hayo ya naweza kutumia kuendeleza miundombinu ya Afya, Elimu na Barabara.
“Niwaombe Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wataalamu wetu kuhakikisha mnasimamia vizuri Ardhi isivamiwe kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya na Barabara hivyo maeneo hayo yatasaidia katika utekelezaji wa miradi hiyo ya Maendeleo hivyo muhakikishe watu hawavamii maeneo na Nyie viongozi wa Serikali za Mitaa msigawe maeneo sio kazi yenu.”
Vilevile Ametoa wito kwa Wananchi iwapo watakua na kero zao wasisite kufika ofisi za Mkuu wa Wilaya pamoja na ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kusaidiwa kutatua Kero hizo kwani kazi yao kubwa ni kuwatumikiaa Wananchi na kuhakikisha wanapata huduma muhimu kwa ukaribu zaidi.
Mwisho wananchi na viongozi wa Kata ya Pugu wamepongeza ziara ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwakumbuka katika kusikiliza kero zao na kumuhakikishia kutekeleza yote aliyoyaagiza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.