Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewaelekeza wahandisi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wataalamu kutoka TARURA kuhakikisha wanaanza mikakati ya kuboresha maeneo yaliyoathiriwa na mvua katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo Novemba 7, 2023 wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, maeneo hayo ni pamoja na eneo la Shule ya Sekondari Dar es Salaam ambalo mifereji ya barabarani inapojaa maji huingia shuleni nakuathiri maeneo ya shule, eneo la daraja linalounganisha Mtaa wa Mwanagati na Magole ambapo daraja hilo limekatika hivyo wananchi kushindwa kuvuka, eneo la daraja linalounganisha Mtaa wa Bangulo na Pugustesheni ambapo daraja hilo lililojengwa kwa ufadhali wa TAMAZAMA Pipelines limeanza kukatika hivyo kupelekea mazingira hatarishi kwa wananchi pindi wanpotumia Daraja hilo huku eneo lingine likiwa ni Zahanati ya Kipawa ambapo maji huoneka kujaa wakati wa mvua.
"Nawapa pole wananchi kwa adha mnayoipata kipindi hichi cha mvua hivyo tunaagiza kujemgwe daraja la mawe lenye midomo nane na kazi hiyo itaanza mara baada ya mvua kupungua hivyo sisi kama Halmashauri tutashirikiana na wataalamu kutoka TARURA kwaajili ya kuimarisha Daraja na wakati huohuo tunajipanga kuimarisha daraja na kujenga daraja litakalo dumu muda mrefu kwaajili ya kuwasaidia wananchi pia niwaombe wananchi mshirikiane na wataalamu wetu katika kukamilisha hili." Amesema Mhe. Mpogolo
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.