Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kudhibiti kuvuja kwa kinyesi katika mfumo wa maji taka katika Mtaa wa Kisiwani, Buguruni, jijini Dar es Salaam
Mhe. Mpogolo ametoa maagizo hayo leo Septemba 3, 2024 wakati wa ukaguzi katika eneo hilo kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu DAWASA baada ya chemba za mfumo huo kufurika kinyesi na kuleta adha kubwa.
Aidha, amegiza mamlaka hiyo, kufumua mfumo huo baada ya kubaini umejengwa chini ya kiwango.
“Natoa wiki mbili kwa DAWASA , kurekebisha mfumo huu wa majitaka. Dhamira ya serikali yetu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga mradi huu siyo kuwaletea adha wananchi bali ni kuwaondolea kero.” amesema Mhe. Mpogolo.
Aidha, amesema amezungumza na Mkrugenzi Mtendaji wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, kufika katika eneo hillo kuukagua mradi huo na kujiridhisha juu ya ubora wake.
“Bwire atakuja hapa kesho akague mradi huu na kujionea hali hii. Pia aangalie ubora wa mradi . Najua ni msikivu na ni mtendaji mzuri.” amesema.
Aidha, amesema miongoni mwa changamoto alizobaini katika mradi huo ni kujengwa kwa kiwango cha chini, ikiwa ni pamoja na mabomba madogo ya kupitisha maji taka yasiyoendana na wingi wa wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya huyo, alionya vikali wananchi kutupa taka ngumu katika chemba za mradi huo hali inayosabababisha kuziba na kuvujisha maji taka.
Kwa upande wake Afisa wa DAWASA, Charles Makoye, aliwaomba radhi wananchi wa eneo hilo, huku akieleza chanzo ni baadhi ya wananchi hao kutupa taka ngumu katika mfumo huo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.