• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

DC Mpogolo awataka walimu wa mkataba kuzingatia nguzo za Utumishi wa Umma

Posted on: April 16th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Edward Mpogolo amewataka walimu wa ajira za mkataba walioajiriwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuzingatia nguzo 5 za utendaji, na kuwa wazalendo kwa Nchi katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo ameyasema Leo tarehe 16 Aprili, 2024 katika kikao kilichojumuisha Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na walimu wa ajira za mkataba katika Ukumbi wa Arnatoglou kwa lengo la kuwaasa na kuwaelekeza walimu wa mkataba yale wanayopaswa kwenda kuyafanya wakiwa kazini. 

Akiongea na walimu wa mkataba Mhe. Mpogolo amesema “Natoa pongezi kwa walimu walioajiriwa na Halmashauri yetu, nawaasa muitumie nafasi hii mliyoipata kwa kuishi katika nguzo 5 ambazo ni kujua jukumu lako kwa watoto, kujifunza kuishi na kuendana na jumuiya inayokuzunguka, kujua mwajiri wako anataka nini, kujua jukumu lako kama mwalimu, na kujua wajibu kwa Taifa lako. Pia nawaomba mkaongeze juhudi na bidii katika ufundishaji ili kupandisha ufaulu katika shule ili Jiji letu liendelee kuwa kinara katika Elimu."

Aidha, Akiongea katika kikao kazi hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa jitihada anazozifanya za kuboresha Elimu katika Jiji la Dar es Salaam huku akimuhakikishia kutekeleza yale yote aliyoyaagiza.

Naye, Kaimu Afisa Elimu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Doreen Masawe ameeleza kuwa “Nipende kumshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa kuajiri walimu 150 wa mkataba katika masomo ya sayansi kwani kutokana na ajira hizo changamoto ya ufaulu katika masomo ya sayansi itakua imetatuliwa kwa kiasi hivyo Nipende kuwahakikishia kupitia ajira hizi ufaulu utazidi kuongezeka zaidi katika Halmashauri yetu."

Aidha, akimwakilisha Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Fidea Mapunda amewakumbusha walimu wajibu wao katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu kwa kutimiza majukumu yote ya kitaifa na kijamii kwa kuwalea watoto kwa maadili ya kinidhamu pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ikiwemo utoaji wa huduma Bora bila upendeleo, pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kwa wakati katika ubora unaotakiwa kwani walimu ndio kioo cha maadili nchini ambapo kwa kuzingatia hayo  sekta ya Elimu nchini itazidi kuimarika.

Akiongea kwa niaba ya Afisa udhibiti ubora wa Shule Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Pudensiana Justine Kisela abeles kuwa “Kikao hichi ni muhimu sana kwenu katika kuhakikisha sekta ya elimu katika Halmashauri yetu inakua kwa kasi hivyo niwaase Waalimu muwe wabunifu kuwajengea wanafunzi uwezo mkubwa wa kufikiri na sio kukariri tu kwaajili ya mitihani. Pamoja na hayo nitoe wito kwa Wakuu wa Shule kuhakikisha mnasimamia walimu wengine kutumia zana za kazi pamoja na kuandaa azimio la kazi Ili kuandaa andalio la somo kama Wizara inavyoelekeza lengo likiwa ni kuleta wepesi wakati wa kufundisha."

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.