Na: Hashim Jumbe, Mkoani Tabora
TIMU ya UMITASHUMTA Mkoa wa Dar es Salaam wameibuka kidedea katika Mashindano ya 27 ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Mwaka 2023 baada ya kumaliza Mashindano wakiwa Washindi wa Pili huku wakijikusanyia Jumla ya Alama 132.
Katika Mashindano hayo Mkoa wa Dar es Salaam wameshika nafasi hiyo huku wakiwa wameshinda Ubingwa wa Mpira wa Mikono Wavulana.
Michezo mingine ambayo Mkoa wa Dar es Salaam wameweza kuchukua vikombe ni Mpira wa Miguu Wavulana waliyoshika nafasi ya pili sambamba na Mpira wa Miguu Maalum na Mpira wa Kikapu Wavulana
Aidha, kwa upande Mpira wa Mikono Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam umeshika Nafasi ya Tatu, hivyo kufanya jumla ya vikombe walivyoshinda kuwa Vitano (5) na kupata Medali Mbili (2) kutoka kwenye mchezo wa riadha
Mashindano hayo ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2023 yaliyoanza tangu tarehe 03 Juni, 2023 Mkoani Tabora yamehairishwa mchana wa leo kwenye viwanja vya Shule ya Wavulana ya Tabora na Mgeni rasmi Mhe. Omary Kipanga, ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Akiongea wakati wa hafla ya kuhairisha mashindano, Mhe. Omary Kipanga alisema "Niwapongeze Wanamichezo wote kwa kuonesha vipaji vyenu katika mashindano haya, ndugu zanguni hongereni sana"
Itakumbukwa kuwa Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 06 Juni, 2023 kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na yalihusisha jumla ya Wanamichezo Wanafunzi 3,164 ambapo Wavulana walikuwa ni 1,633 na Wasichana 1,531.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.