• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Elimu zaidi yatolewa kuhusu lishe bora pamoja na usalama wa chakula

Posted on: August 31st, 2023

Maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi na mpangilio bora wa vyakula ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa yanayoweza kuwapata mara kwa mara.

Elimu hiyo imetolewa Leo tarehe 31 Agosti, 2023 katika siku ya Afya na Lishe kwa Kata ya Jangwani kwenye Mkutano uliowashirikisha Maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Viongozi wa Kata na Mitaa, Wananchi na wadau mbalimbali wa Afya pamoja Lishe.

Mbali na kufundisha kuhusu mpangilio bora wa mlo kamili somo lililofundishwa na Bi. Neema Mwakasege, wananchi pia walipata fursa ya kufundishwa namna ya kuandaa chakula cha mtoto mwenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea ambapo Bi. Neema Manyama aliandaa uji wenye makundi matatu ya vyakula ambayo ni nafaka, maziwa pamoja na sukari.

Aidha, suala la lishe bora linakwenda sambamba na usafi pamoja na usalama wa chakula kuanzia shambani kinapotoka mpaka muda wa kuliwa. Bi. Safiona Mdee ambaye ni Afisa Lishe wa Kata ya Jangwani amesema kuwa ili chakula kiwe Safi na salama lazima taratibu na kanuni za usafi wa chakula zifuatwe.

"Ni vyema kuzingatia kanuni na taratibu za usafi na usalama wa vyakula hupita maeneo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa sio salama kabla ya kumfikia mlaji mfano sokoni ambapo uhifadhi wake unaweza kuwa si salama au shambani ambapo nafaka hupulizwa dawa za kuua wadudu ili zisiharibike haraka hivyo kufanya vyakula hivyo kuwa hatarishi kutumiwa moja kwa moja na mlaji bila kuchukua tahadhari yoyote." Amesema Bi. Mdee

Kwa upande wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wamewashukuru wataalamu kwa masomo mazuri waliyoyatoa kwao na kuwafanya wajifunze mambo mengi waliyokuwa hawayafahamu kuhusu lishe bora na kutoa wito kwa wananchi wa maeneo mengine kujitokeza kwa wingi pale Maafisa Lishe wanapowatembelea katika mitaa yao.    

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.