Na: Doina Mwambagi
Asali ni moja ya vyakula vya asili vinavyotambulika kwa kuongeza afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume. Virutubisho vilivyomo kwenye asali huchochea mzunguko mzuri wa damu, kuimarisha homoni za uzazi na kuongeza nguvu asilia za mwili.
Matumizi ya mara kwa mara ya asali safi husaidia pia kupunguza matatizo ya uchovu, kushuka kwa nguvu, na huchangia kuongeza uhai wa seli za uzazi.
Haya yamewekwa bayana na na Mkurugenzi wa kikundi cha Pishon Honey, kinachojihusisha na uchakataji wa asali safi, ambacho kwa sasa kinashiriki maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Morogoro.
Kikundi hiki ni mnufaika wa mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, fedha ambazo zimekiwezesha kuongeza uzalishaji, kuboresha vifungashio na kufikia masoko mapya.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Kikundi cha Pishon Honey, Bi. Jackline Mabere, amesema: “Tunashukuru Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutuwezesha kupitia mkopo wa asilimia 10. Fedha hizi zimetusaidia kuongeza uzalishaji, kuboresha vifungashio na kuongeza ajira kwa vijana. Tunahamasisha Watanzania kutumia asali safi kwa kuwa ni kinga na tiba ya magonjwa mengi, ikiwemo kuimarisha afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume.”
Pishon Honey huuza asali safi ya nyuki wa asili, isiyochanganywa na kemikali. Kikundi kinapanga kuongeza thamani kwa kuzalisha bidhaa mpya zitokanazo na mazao ya nyuki ili kusaidia wafugaji nyuki wa ndani na kuimarisha uchumi wa kaya.
Ushiriki wa Kikundi cha Pishon Honey katika maonesho ya Nanenane ni mfano halisi wa jinsi mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inavyosaidia kuinua vikundi vya wajasiriamali wadogo na kuimarisha afya ya jamii kupitia bidhaa za asili.
“CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI 2025”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.