• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Halmashauri ya Jiji la DSM yaibuka kinara ukusanyaji mapato ya ndani kwa kipindi cha nusu mwaka 2019/2020

Posted on: February 9th, 2020

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeibuka kidedea katika ukusanyaji mapato ya ndani katika kipindi cha nusu mwaka (Julai-Desemba, 2019) kwa Halmashauri za Majiji nchini baada ya kukusanya mapato yake ya ndani kwa asilimia 71 ya makisio yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Akizungumzia ukusanyaji wa mapato hayo Waziri Jafo amesema kwa mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri zilipanga kukusanya shilingi za Kitanzania bilioni 765.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na kipindi cha nusu mwaka (Julai hadi Desemba, 2019) Halmashauri zimekusanya jumla ya shilingi za Kitanzania bilioni 356.81 ambayo ni asilimia 47 ya makisio ya mwaka.

Alifafanua kuwa taarifa za mapato ya vyanzo vya ndani katika kipindi cha Julai - Desemba, 2019 umeonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato yaliyokusanywa kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 56.7 ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho cha Julai - Desemba, 2018 sawa na ongezeko la asilimia 19.

“Uchambuzi unaonesha kuwa Halmashauri 63 kati ya Halmashauri 185 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 50 na zaidi ya makisio kwa mwaka wa fedha 2019/20 na Halmashauri mia ishirini na mbili (122) zimekusanya mapato ya ndani chini ya asilimia 50 ya makisio ya mwaka.

Aidha, Halmashauri hukusanya mapato mengi au kidogo kwenye vyanzo tofauti kulingana na hali halisi ya shughuli za kiuchumi za kila Halmashauri hivyo, ongezeko hilo limetokana na sababu mbalimbali ikiwemo ushuru wa zao la korosho katika Halmashauri za Mikoa ya Mtwara na Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita (Julai – Desemba, 2019), Halmashauri za Wilaya za Tunduru na Kibondo zimekusanya mapato kwa asilimia 104 ya makisio ya mwaka 2019/2020.

Pia Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zote zilizokusanya zaidi ya asilimia 100 hadi Desemba, 2019 na zile ambazo zimejitathmini na kuona upo uwezekano wa kuzidi asilimia 100 ya bajeti za mapato ya ndani ifikapo Juni, 2020 zinaelekezwa kufanya mapitio ya bajeti kwa mujibu wa Sheria ya bajeti ya mwaka 2015 ili ziweze kuongeza bajeti za mapato na matumizi ya fedha hizo.

Jafo alisema katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi za Kitanzania bilioni 29.75 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi za Kitanzania milioni 186.10”, alisema Jafo

Akifafanua ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kimkoa kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo amesema Mkoa wa Geita umefanya vizuri ambapo umekusanya wastani wa asilimia 63 ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo.

Aidha, Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Tanga ambao umekusanya wastani wa asilimia 36 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Pia Waziri Jafo ameweka  wazi ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kukusanya kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 83.86 na  Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Katavi ambao umekusanya shilingi za Kitanzania bilioni 4.68.

Akifafanua ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa kuzingatia aina ya Halmashauri kwa kigezo cha asilimia ya makusanyo ukilinganisha na makisio Waziri Jafo amesema kwa upande wa Majiji Jiji la Dar es Salaam limeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 71 ya makisio yake na Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya kwa asilimia 41 ya makisio yake ya mwaka.

Upande wa Manispaa, Ilemela imeongoza kundi hilo kwa kukusanya asilimia 75 ya makisio yake na Manispaa ya Kigoma imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya kwa asilimia 26 ya makisio yake.

“Katika Halmashauri za Miji, Mji wa Njombe umeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 88 ya makisio yake ambapo Halmashauri ya Mji wa Babati imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 30 tu” alisema Jafo.

Aidha, kwa kundi la Halmashauri za Wilaya amesema  Wilaya za Tunduru na Kibondo zimeongoza kwa kukusanya asilimia 104 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2019/20 wakati Halmashauri za Mafia, Ukerewe na Gairo zimekuwa za mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya asilimia 18 ya makisio.

Waziri Jafo aliongeza kuwa kwa upande wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia aina za Halmashauri kwa kigezo cha wingi wa makusanyo Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya shilingi za Kitanzania bilioni 29.75 na Jiji la Dar es Salaam limekuwa la mwisho kwa kukusanya shilingi bilioni 6.03.

“Halmashauri za Manispaa, Ilala imeongoza kwa kukusanya shilingi za Kitanzania bilioni 29.13 na  Manispaa ya Kigoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya shilingi za Kitanzania milioni 694.93.

Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa wingi wa mapato katika Halmashauri za Miji ambapo imekusanya shilingi za Kitanzania bilioni 4.64. Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya shilingi za Kitanzania milioni 459.44” alisema Jafo.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya, Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi kwa Halmashauri za Wilaya ambapo imekusanya shilingi za Kitanzania bilioni 3.89 na Wilaya ya Bumbuli imekuwa ya mwisho kwa kukusanya shilingi za Kitanzania milioni 186.08.

Waziri Jafo alimalizia kwa kuzitaka Halmashauri zote kuendelea kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki na kudhibiti ukusanyaji wa fedha na mbichi na ameweka wazi kuwa taarifa ya mwisho ya kota ya nne ya ukusanyaji wa mapato ya ndani sambamba na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ataitoa tarehe 18.06.2020 kabla ya Bunge kuvunjwa hivyo kila mtu ahakikishe anatekeleza jukumu hili kwa ufanisi ili kufikia malengo.

KWA MCHANGANUO ZAIDI FUATA VIUNGANISHI VIFUATAVYO HAPA CHINI...

http://dcc.go.tz/storage/app/uploads/public/5e4/186/b97/5e4186b97dab2000439583.pdf

http://dcc.go.tz/storage/app/uploads/public/5e4/186/760/5e4186760b837212955560.pdf

http://dcc.go.tz/storage/app/uploads/public/5e4/186/347/5e41863477ea7434403877.pdf

http://dcc.go.tz/storage/app/uploads/public/5e4/185/da8/5e4185da8dad1013123550.pdf

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.