Na: Shalua Mpanda
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amesema atahakikisha miradi yote ya maendeleo iliyosimama kutokana na sababu mbalimbali inaendelea ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Wananchi.
Ameyasema hayo leo hii Novemba 11, 2024 wakati akijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mabelya amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata nafuu ya maisha kwa kutekeleza miradi mbalimbali itakayosaidia kupata huduma kwa urahisi.
“Tunataka Miradi inayoonekana,si miradi ya kwenye madaftari wala miradi ya kwenye kompyuta. Miradi hii si ya kwangu wala ya Mheshimiwa Meya ni miradi ya wananchi na tunataka Miradi yenye tija" .Aliongeza Mkurugenzi Mabelya.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyu wa Jiji amesema kwa kutambua umuhimu wa miradi hiyo wameamua kufuta mkataba na baadhi ya wakandarasi ambao walikuwa wakikwamisha ukamilishaji wa Miradi.
Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine, baadhi ya waheshimiwa madiwani wamezungumzia umuhimu wa Halmashauri hii kuwa na mambo wake wa kutengeneza barabara (greda), utakaosaidia kufanya ukarabati wa baadhi ya barabara zenye changamoto hasa wakati wa mvua.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.