Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Viwanda, Biashara naUwekezaji inaendelea kuhakikisha huduma za kibiashara hususani utoaji wa leseni za biashara zinawafikia wananchi kwa wakati na mahali walipo, hayo yamebainishwa leo Septemba 18, 2023 na Mkuu wa Divisheni hiyo wakati wa zoezi la utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.
Akiongea wakati wa zoezi hilo litakaloendeshwa kwa mwezi mmoja, Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Nickas Msemwa ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la DSM imedhamiria kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa ukaribu zaidi kwani wameweza kuanzisha kanda saba za kutolea huduma pamoja na kutoa leseni kwa wafanyabiashara kwa kuwafuata katika maeneo yao ya biashara.
Sambamba na hilo Bw. Msemwa ameesema “Zoezi hili limedhamiria kuwafikia wafanya Wafanyabiashara zaidi ya elfu 15 kwa Kariakoo ambao mpaka sasa wafanyabiashara elfu nane bado hawajapata leseni hivyo mpango mkakati huu wa kuleta huduma karibu yao utasaidia kukamilisha zoezi hili ambapo kwa Kariakoo zoezi hili litaendelea kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo tutaelekea kanda za pembezoni ila ikumbukwe kuwa utoaji huu wa leseni umeambatana na elimu ya jinsi ya kujisajili kwenye mfumo na namna gani ya kutumia mashine zetu katika utoaji wa risiti hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashata wote kutumia fursa hii kujipatia leseni ya biashara papo hapo bila kusubiri na kwa Wafanyabiashara wote wenye taarifa hizi wafike maeneo ya huduma ili wapate leseni zao pamoja na elimu kwa ujumla.”
Akitoa wito kwa Wafanyabiashara wenzake Bw. Julius Joseph Lullenge ametoa shukrani zake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalamu wake kwa kuona tija kuhusu swala la leseni na kuwasogezea huduma hiyo karibu huku akiwahimiza wafanyabiashara wenzake kufika eneo la utoaji huduma na kupata elimu ya namna ya kutumia mashine kwani yeye amefika mahali hapo na ameweza kuelekezwa namna ya kutoa risiti kwa kutumia mashine za EFD na kuweza kuelewa pia ametoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kutumia fursa kwa kupata leseni papo hapo na kujifunza kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.