Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, leo tarehe 25 Oktoba,2022 wametoa mafunzo ya huduma ndogo za fedha (Vicoba na Saccos) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na wahamasishaji (Promoters) katika Ukumbi wa Anatoglou, jijini Dar es Salaam yenye lengo la kujenga uelewa wa pamoja katika utendaji kazi wao na kuhimiza ushirikiano kati ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na wahamasishaji (Promoters) na kuongeza ufanisi wa kufanya shughuli za huduma ndogo za fedha kwa kuhimiza utoaji wa taarifa na kufanya kazi zao kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi.Tabu Shaibu ametoa shukrani za dhati kwa kazi kubwa inayofanywa na wahamasishaji wa huduma za fedha kwa Jiji la Dar es Salaam na maafisa Maendeleo ya Jamii katika kuchochea uanzishwaji,uimarishaji na uendelezaji wa huduma ndogo za fedha.
Aidha amewataka maafisa hao kuwa wabunifu katika utendaji kazi wao.
Pia amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea na jitihada zake kubwa za kuwaletea Maendeleo wananchi.
Akiongoza mafunzo hayo Mratibu wa mafunzo kutoka Jiji la Dar es Salaam, Bi.Happiness Joachim, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kufanya kazi kazi kwa bidii na weledi ili kufikia matarajio katika kuimarisha vikundi vilivyopo kuwa Saccos na Saccos kuwa benki za jamii.
Huduma hizo ndogo za fedha zinawawezesha wananchi kujiwekea akiba na kupata mikopo nafuu kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujiongezea kipato na kujikwamua na umaskini.
Nao washiriki wa mafunzo wameshukuru kupata elimu ya mafunzo ya huduma ndogo za fedha na kuahidi kuwa watatekeleza yale yote waliyofundishwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.