Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo, tarehe 21 Julai 2025, imepokea ugeni kutoka CAMFED Tanzania waliokuja kwa lengo la kujadili maendeleo ya wanafunzi wa kike wanaonufaika na mpango wa shirika hilo katika sekta ya elimu.
Wageni hao wamekutana na Mkurugenzi wa Jiji, Ndugu Elihuruma Mabelya, na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu ushirikiano.
Mkurugenzi Mabelya amepongeza mchango wa CAMFED na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mashirikiano kati ya shirika hilo na Halmashauri ya Jiji, ili kuimarisha juhudi za serikali katika kuwawezesha watoto wa kike kielimu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.