• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Jiji la DSM latekeleza Sera ya utoaji huduma ya Chakula na Lishe mashuleni

Posted on: February 6th, 2023

Suala la usomaji shuleni linahitaji wanafunzi kuwa na afya bora na utimamu wa akili, hivyo wanafunzi wakipata chakula shuleni itawasaidia kujenga afya bora na hivyo kumudu kuelewa yale wanayojifunza shuleni na kufanya matokeo yao na ufaulu kwa ujumla kuwa wa juu.

Mnamo tarehe 29 Octoba, 2021 Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Teknolojia ilizindua muongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma za chakula na lishe kwa wanafunzi mashuleni wenye lengo la kuwaelekeza wadau wa elimu nchini kote namna bora ya kutekeleza utoaji wa huduma ya chakula na lishe mashuleni.

Katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Muongozo huo umepokelewa kwa muitikio chanya kwani shule nyingi zimeanza kutoa huduma ya chakula mchana na kuwawezesha wanafunzi kuzingatia masomo yao kikamilifu. Shule ya Sekondari Jamhuri ni moja ya shule ambazo zimeanza kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi wake. Na kutokana na maelezo ya Mkuu wa shule hiyo Mwl. Boniphase Mwalwego amesema kuwa kuanzishwa kwa huduma ya chakula katika shule yake kumesaidia sana hali ya ufaulu kuwa juu hasa kwa wanafunzi wa kidato cha pili na kidato cha nne waliofanya mitihani yao ya Taifa mwaka jana wa 2022.

“Asilimia 75 ya wanafunzi wa kidato cha pili katika shule yetu wamepata ufaulu wa daraja la kwanza, na katika wanafunzi wote waliofanya mtihani huo hakuna aliyerudia kidato. Kwa upande wa Kidato cha nne asilimia 80 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo wamepata daraja la kwanza.” Amesema Mwl. Mwalwego

Aidha amesema kuwa huduma ya chakula na lishe mashuleni inasaidia kujenga akili za wanafunzi kikamilifu. Kwa sababu hivi sasa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani wanaanza masomo yao saa 1 asubuhi, hivyo sio rahisi kwa wao kupata chakula nyumbani kabla ya kwenda shule. Kupata chakula shuleni kunawasaidia wanafunzi kuwa wasikivu na kuzingatia kile wanachofundishwa wawapo darasani na mazingira ya shule kwa ujumla.

Vilevile utoaji wa chakula umepunguza kasi ya utoro kwa wanafunzi na kuwapa motisha ya kusoma. Hapo awali wanafunzi walikuwa na tabia ya kutoroka kabla ya vipindi kuisha kutokana na njaa, lakini kufuatia kuanzishwa kwa huduma ya chakula katika shule yao, wanafunzi wamekuwa wakihudhuria vipindi vyote darasani na kuachana na tabia ya utoro.

Mwl. Mwalwego pia amesema kuwa kwa miaka inayoendelea ana Imani kuwa uanzishwaji wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe mashuleni utaongeza hali ya ufaulu zaidi kwa wanafunzi wao kwani akili zao zinajengeka kwa kupata lishe kwa wakati katika muda wote wawapo katika mazingira ya shule.

Sambamba na hilo wanafunzi wa shule hiyo wametoa shukrani zao za dhati kwa Serikali kwa kuanzisha muongozo huu wa chakula na lishe mashuleni, kwani umekuwa ni chachu kubwa na umesaidia kuleta hamasa kwa wanafunzi katika mchakato mzima wa kusoma na kujifunza.

Ikumbukwe kuwa moja ya vitu ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amevipa kipaumbele ni suala la Lishe bora nchini. Na hii ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha nchi inaondokana na tatizo la utapiamlo na wananchi wake wanakuwa na afya bora na kuwawezesha kufanya kazi kwa bidi kwa maslahi mapana ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa zima kwa ujumla.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru waweka jiwe la Msingi Kituo cha Afya Mzinga

    June 03, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wakagua mradi wa vijana "Ulipo Tupo" Tabata

    June 03, 2025
  • Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Magengeni - Chang'ombe umewekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa

    June 03, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wazindua mradi wa Nishati Safi Soko la Samaki Feri

    June 03, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.