Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na wataalamu wa Biolojia Molekuli na Bioteknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo tarehe 13 Juni, 2023 imefungua mafunzo kwa Maafisa Ugani ya Uzalishaji wa mbegu bora za Uyoga katika Kituo cha Rasilimali Kilimo kilichopo Pugu - Kinyamwezi.
Akifungua mafunzo hayo Diwani wa Kata ya Pugu Mhe. Imelda Samjela amesema "Umuhimu wa zao hili la uyoga kwa wananchi kupitia mafunzo haya naamini yataleta matokeo makubwa kwa wataalamu wetu katika kufungua njia ya biashara kwa wananchi pia kusaidia kama tiba na mboga katika familia zetu.
Namshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni hii ya Kilimo katika kuongeza thamani ya kilimo kwa maeneo ya Mjini na Kata ya Pugu imekuwa sehemu kubwa kupitia kituo hiki cha rasilimali za kilimo"
Aidha, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Fredrick Mshote amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa mfano wa kuigwa kwenye sekta ya Kilimo kwani katika kituo hiki kimekuwa chachu ya kuzalisha wakulima wenye weledi na kuweza kufanya shughuli hii ya kilimo "Kituo hiki kimewahi kushinda tuzo ya kuwa kituo bora mwaka 2009. Hivyo basi nashukuru uongozi wa kituo hiki kwa kuendelea kukiimarisha kwa maana ya kuzalisha wakulima wenye weledi zaidi"
Naye, Afisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi Sije Lebi amesema "Matarajio ya mafunzo haya kwa maafisa kilimo wanaoshiriki ni kuweza kufikia hatua ya kuwa wajuzi wa kuzalisha uyoga huu kwa madhumuni ya kukuza na kuimarisha kipato cha wakulima kwani kwa sasa wakulima 40 wanatarajiwa kunufaika nao kupata ujuzi baada ya mafunzo haya."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.