Mkuu wa Wilaya ya Illala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Ilala kuhakikisha wanakua mstari wa mbele kuwaelimisha wanawake kuhusu muongozo mpya wa utoaji wa mikopo.
Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo Oktoba 15, 2024 wakati wa kikao cha viongozi wa majukwaa kwa Kata 36 za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kikiwa na lengo la kutoa elimu ya muongozo mpya wa utoaji mikopo pamoja na uhamasishaji wa kujiandikisha na kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
Akiongea na viongozi hao, Mhe. Mpogolo amewahimiza viongozi hao kuhakikisha elimu wanayopewa wanaenda kuelimisha wananchi huku akiwataka wawe makini katika kusimamia vikundi na wasianzishe vikundi vipya kwani nikinyume na sheria na ikibainika wamefanya ivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
"Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha viongozi wote wanaosimamia vikundi vya mikopo wanapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utoaji na usimamizi wa mikopo kwa kutumia mfumo mpya hivyo ninyi kama viongozi wa majukwaa mnatakiwa kuwaelimisha wananchi hususani wanawake kutumia fursa hii katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kwani mikopo ya awamu hii inatolewa kuanzia laki tano hivyo haya wafanyabiashara ndogondogo wanafursa yakupata mikopo hii hivyo ni imani yangu mtawawlimisha vyema na hamtafanya kazi kinyume na sheria." Ameeleza Mhe. Mpogolo.
Halikadhalika, Mhe. Mpogolo amewahimiza viongozi hao kuhakikisha wanajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura la uchaguzi wa Serikali za Mitaa Oktoba 11 na linahitimishwa Oktoba 20, 2024 ili waweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27, 2024.
Awali Akitoa Mafunzo kwa wananchama hao Mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi Halmshauri ya Jiji la DSM Bi. Georges Asenga wanachama hao amesema mafunzo ya muongozo mpya wa utoaji na usimamizi wa mikopo kwa njia ya benki huku akiwasisitiza viongozi wa Jukwaa hilo kuhakikisha wanakua makini katika kuomba mikopo pamoja na kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuchukua mikopo kulingana na biashara zao ili kuepuka usumbufu wakati wa Marejesho.
Sambamba na hilo, Bi. Asenga amemshukuu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwakua mikopo hiyo itakua chachu ya kuwakwamua wananchi kiuchumi huku akitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hii kuweza kujitokeza katika mafunzo ya utoaji wa elimu ili waweze kuwa na uelewa na hatimaye kutengeneza vikundi na kupata mikopo isiyo na riba itakayo waondoa kwenye wimbi la umaskini.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilayabya Ilala Bi. Rehema Sanga ametoa shukrani zake kwa kupatiwa elimu hiyo huku akimuhakikishia Mkuu wa Wilaya kutekeleza yale yote aliyowaelekeza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.