• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala wafanya ziara Idara ya Elimu Sekondari Jiji la DSM

Posted on: January 17th, 2023

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala ameridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa upande wa Idara ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, hayo ameyabainisha leo Januari 17, 2023 katika ziara yake na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Ilala walipojadiliana mambo mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha Elimu ya Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Ufundi ikiwepo Elimu ya Watu Wazima.

Akiongea katika ziara hiyo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Mtiti Mbassa Jirabi ameeleza kuwa "Lengo la kuja hapa ni kuhakikisha tunapata maelezo sahihi na ya kina kama sehemu ya kujifunza ili tukatoe elimu kwa wanachama wetu wa Jumuiya ya Wazazi inayosimamia Elimu, Malezi, Mazingira, Afya pamoja na Utamaduni.”

Aidha, Ndugu Mbassa aliendelea kusema “Kama kamati ya utekelezaji tunaridhishwa na mwenendo wa Elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lakini pia ombi letu kubwa tunaomba utoro mashuleni ushughulikiwe pamoja na mwenendo wa maadili kwa wanafunzi wa rika huku tukiwataka wanafunzi wenye mahitaji maalumu kupewa kipaumbele ili waweze kusoma katika mazingira rafiki kama wanafunzi wengine.”

Naye Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mwl. Mussa Ally amesema “Kipekee napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuboresha sekta ya Elimu Nchini kwani amekua akifanya jitihada za juu sana kuhakikisha anatoa fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaofaulu kwenda Sekondari waweze kusoma katika miundombinu rafiki ili kukuza sekta ya elimu nchini.”

Sambamba na hilo Mwl. Mussa ameeleza kua katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ibara ya 80 kipengele ‘A’ inaangalia watoto wa Tanzania wote wenye uhitaji wa kupewa elimu wapewe fursa na Elimu hiyo iwe bora na yenye mafanikio kwa watoto wetu hivyo kutokana na kifungu hicho, Halmashauri ya Jiji la DSM kupitia Idara ya Elimu Sekondari wameweza kutekeleza hilo.

“Niwahakikishie tu kwamba kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Chama sisi kama Idara ya Elimu Sekondari tutahakikisha wanafunzi wanasoma kwa bidii katika mazingira rafiki na pia tutahakikisha tunaukomesha utoro kwa kushirikiana na viongozi wote kuanzia ngazi ya Kata pia hatutaishia humo kwani kwa watoto watakaopata mimba mashuleni wataendelea na masomo kwa kuendelea kusoma elimu ya watu wazima hivyo niwahakikishie tu yakwamba watoto wetu watasoma kwenye mazingira salama na ufaulu utazidi kuongezeka.” alimalizia Mwl. Mussa

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.