Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha Robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha Januari -Machi 2024 ambapo leo Mei 15, 2024 imetembelea miradi mitatu (3) ikiwemo ujenzi wa matundu 20 ya vyoo vya shule ySekondari Kerezange, Ujenzi wa Kituo cha Afya Mzinga na ujenzi wa Madarasa shule ya Sekondari Bonyokwa.
Akizungumza wakati wa majumuisho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala Mhe. Nyansika Getama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam fedha kwaajili ya ukamilishaji na uboreshaji wa miundombinu ya Elimu, Afya na Barabara kwani anatusaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi wa maeneo ya mbali.
Aidha, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bonyokwa Mwl. Arnold Tenganamba amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo kwa juhudi zake za ufatiliaji wa kina wa ujenzi wa shule, na pia kutoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Jiji la DSM kwa kutoa pesa zaidi ya milioni 500, Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo.
Sambamba na hilo , Kamati imeagiza watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana kuhakikisha wanatatua changamoto zinazojitoleza katika miradi. Pia, imewataka Wakandarasi wanaosimamia kumalizia miradi ndani ya muda uliopangwa na kwa usahihi ili kuwapunguzia Wananchi wa maeneo ya jirani adha ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma hizo za kijamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.