Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya kikao cha Robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2022 kilichofanyika leo tarehe 26, Mei 2022 katika ukumbi wa mkutano wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kupitia taarifa ya utendaji kazi na utekelezaji wa afua za lishe za Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Afya, Mifugo, Maji, Maendeleo ya Jamii na Vijana, Elimu Msingi na Sekondari, MDH pamoja na vyombo vya habari wa Kamati hiyo.
Akiongoza Kikao hicho cha Lishe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Jiji la Dar es Salaam Bi.Tabu F. Shaibu ameeleza kuwa Kamati ya Lishe ni Kamati muhimu inayotekeleza na kusimamia ulaji na uandaaji wa lishe bora kwa afya za Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kilimo, Umwagiliaji na Ushiriki kwa niaba ya Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Vernice Malisa alieleza kua Idara imeweza kuhamasisha Wakulima 484 waliopo kwenye mabonde ya Kata za Msongola, Zingiziwa, Chanika, Kivule, Buyuni, Ukonga, Gongolamboto na Kitunda kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mboga mboga ifikapo June, 2022.
Aidha Bi. Malisa aliendelea kueleza kuwa katika kuhakikisha Wananchi wanapata mboga mboga salama Idara imeendelea kutoa elimu na kuhamasisha kilimo cha Magorofani ambacho hutumia eneo dogo katika uzalishaji kwani mbogamboga hupandwa katika mifuko ya Salfet na makopo ambayo hayachukui nafasi kubwa ambapo wakulima waliweza kuhamasishwa kuhusu matumizi ya Teknolojia ya kilimo bora ili kuongeza upatikanaji wa chakula cha kutosha chenye lishe bora na Salama kwa mlaji kupitia Shamba Darasa MOJA la mboga katika kiyuo cha Kata cha Rasilimali Kilimo Kinyamwezi.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bibi. Neema Mwakasege alieleza kuwa Kamati itafanya ziara ya mafunzo ya kilimo katika kituo cha Shamba DARASA MOJA la mboga katika Kituo cha Kata cha Rasilimali KIlimo Pugu Kinyamwezi ili kujifunza kilimo cha Magorofani na namna bora ya utayarishaji wa upandaji mbogamboga kwa njia salama ambapo kamati itakua na jukumu la kuelimisha jamii ikijikita katika shule za msingi na sekondari ili wanafunzi hao waweze kufikisha Elimu hiyo katika Jamii inayowazunguka.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.