Kamati ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yajipanga kuboresha machinjio ndani ya masoko hususani machinjio ya kuku, hayo yamebainishwa leo Mei 14, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa machinjio ndani ya masoko lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo zilizotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoanza Januari hadi Machi 2024.
Wakiwa katika Ziara hiyo, Kamati ilitembelea Machinjio ya Kuku katika Soko la Ilala ambapo kamati iliweza kutembelea machinjio hayo kujionea namna wanavyofanya kazi na mazingira ya kazi kama ni salama kwa afya za Wananchi.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdulkarim Masamaki amesema “Kamati hii imeamua kufanya ziara katika machinjio yaliopo masokoni ili kujionea namna ya utendaji kazi wao pamoja na usafi wa mazingira kwa ujumla kwani bidhaa hizi huwahusu wnanchi moja kwa moja wakiwa kama walaji hivyo lazima tuhakikishe zinatengenezwa mahali safi na salama kwa ajili ya kulinda afya za Wananchi wetu ambapo katika machinjio hii ya Kuku Soko la Ilala tumejionea namna kazi zinavyoenda japo kuna changamoto tumezibaini za ukosefu wa maji lakini bado nyama zinachinjwa katika hali ya usafi hivyo sisi kama kamati tunamuagiza Afisa masoko kuhakikisha matatizo hayo yanatatuliwa kwa wakati.”
Kwa upande wake Afisa Masoko wa Halimashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Buberwa Alex ameihakikishia kamati kutekeleza yote waliyoyaagiza huku akisisitiza kuwa Halmashauri imetenga bilioni 40 kwaajili ya ujenzi wa soko la kisasa Ilala ambalo litakua na eneo la machinjio ya kisasa ya kuku yenye ubora na kiwango cha hali ya Juu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.