Kamati ya Ustawi wa Jamii kutoka Visiwani Zanzibar leo tarehe 8 Novemba, 2022 imefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuja kubadilishana uzoefu katika Idara ya Elimu Maalumu katika Jiji la Dar es Salaam ambapo msafara huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Malindi Mhe. Mohamedi Ahmada Salum pia Mbunge na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally Abdul-Ghulam Hussein.
Wakiwa katika viunga vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa JIji la Dar es Salaam Eng. Amani Mafuru na kuweza kubadilishana uzoefu Kaimu Mkurugenzi wa Jiji anasema “Nachukua nafasi hii kuwakaribisha katika Jiji la Dar es Salaam na tumefarijika kupokea ugeni huu Mkubwa kutoka Zanzibar, hii inatupa uwezo wa kubadilishana uzoefu jinsi ya kuendesha shule maalumu”.
Sambamba na hilo ugeni huo uliweza kutembelea Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo katika Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam kujifunza na kujionea shughuli za kielimu zinazofanyika katika shule hiyo, shule kongwe ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambayo inachukua wanafunzi mbalimbali wenye ulemavu tofauti ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasioona, viziwi wasioona, wanafunzi wenye ulemavu wa akili na ulemavu wa ngozi.
Pia, Ugeni huo ulipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Buguruni Viziwi ambayo ni maalumu kwa kufundisha wanafunzi wasiosikia ili kuwawezesha kufanya mawasiliano ya kila siku pamoja na kupata elimu, mafanikio katika ufundishaji wa shule hiyo umeenda katika mapana makubwa, akiongea Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buguruni viziwi Bw. Yahaya Maftaa anasema
“Shule ya Msingi Buguruni viziwi imefikia mafanikio makubwa kwani wanafunzi wanaoanzia ngazi ya awali mpaka darasa la saba wanakuja hapa hawajui lolote lakini wanatoka hapa wanajua kusoma na kuandika na kuwasiliana kwa lugha za alama pia mpaka sasa tuna wanafunzi watatu ambao wamefika Chuo Kikuu Kutoka hapa”.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii kutoka Visiwani Zanzibar Mhe. Mohamedi Salumu amesisitiza na kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa watendaji wote, walimu, maafisa Elimu kitengo Maalumu kwa kuweza kufanikisha na kuwalea wanafunzi wote wenye mahitaji maalumu tumejifunza vitu vingi sana katika Shule hii ya Uhuru Mchanganyiko pamoja na Buguruni Viziwi kupitia ziara hii. “Kwa hakika sisi kama kamati kwa niaba ya wote tunaishukuru sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ziara hii tumejifunza vya kutosha na tunaimani tumebadilishana uzoefu vya kutosha na kuweza kuyafanyia kazi tukirudi Zanzibar pia Nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha watoto hawa kupata elimu stahiki”
Naye Mjumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Mbunge na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Abdul-Ghulan Hussein amesema
“Lengo letu ni kuja kujionea shule hizi zinavyoendeshwa na kubdilishana uzoefu ili sisi situweze kuendesha na kuzidisha ufanisi kupitia ziara hii pia tunaweza kupata fursa sisi kama Wizara kutuma kamati kuja kujifunza zaidi na kuimarisha ushirikiano”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.