Wananchi zaidi ya elfu tano wanatarajiwa kujitokeza kwenye Uzinduzi wa kampeni ya huduma ya bima afya iliyoboreshwa ili waweze kupata huduma za Afya kuweza kupata elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo afya ya uzazi, huduma ya macho na huduma nyinginezo pamoja na kujisajili katika mfuko wa bima ya afya.
Wito huo umetolewa Januari 21, 2025 na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gerezani na Mwenyekiti wa hamasa wa siku ya uzinduzi wa kampeni ya siku ya kujiunga bima ya afya iliyoboreshwa Dkt. Magreth Mathew wakati akizungumza na City FM itakayofanyika Januari 30, 2025 kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 9:30 alasiri katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Amesema kuwa ni vyema wananchi wajiunge na huduma ya afya mapema ili waweze kuzielewa na kuzitambua kiundani kwaajili ya kuweza kuwa na uhakika wa kupata huduma ya afya kwa uhakika.
Aidha, huduma ya afya iliyoboreshwa (CHF) inapatikana katika ofisi za Serikali za Mitaa na maeneo yote ya kutolea huduma za afya , na baada ya kujisajili tiketi itaanza kutumika papo hapo.
Vilevile amewataka wananchi kuzingatia gharama za bima hiyo ambapo mtu mmoja atalipia shilingi elfu 40 kwa mwaka na kwa familia yenye idadi ya watu sita watalipia laki moja na nusu, halikadhalika katika usajili wa familia ya watu sita inatakiwa kupeleka picha za watu hao sita ili waweze kutambulika.
Amesema watoa huduma ngazi ya jamii watapatiwa Bima ya zaidi ya 277 ili wanapougua wapate matibabu mapema sambamba na makundi maalum watapatiwa Bima 200.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.