• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Kata ya Kipunguni Halmashauri ya Jiji la DSM wafanya tamasha la maonyesho ya wajasiriamali ambao ni wanufaika wa Asilimia 10% ya mapato ya ndani

Posted on: January 27th, 2022

Na. Judith Damas

Uongozi wa Kata ya Kipunguni  kwa kushirikiana  na  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii leo Januari 27, 2022 wameeandaa tamasha la maonyesho  ya wajasiriamali wa Kata ya Kipunguni yaliyofanyika  katika viwanja vya Moshi Bar Kata ya Kipunguni Jijini Dar es salaam lengo likiwa ni  kutambulisha bidhaa zao na kutoa elimu kwa wajasiriamali wanaofanya biashara na wanaotaka kuanzisha biashara zao ambapo  ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004.

Akiongea katika tamasha hilo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Saady Khimji amesema "Kwa niaba ya Mstahiki Meya  Pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam napenda kuwahakikishia wananchi wajasiriamali wa Kata ya Kipunguni Kuwa tutashirikiana nanyi ili kuweza  Kuwawezesha wananchi wetu kujikwamua kiuchumi hususani wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 

Aidha Mhe. Khimji amewapongeza Wajasiriamali wa Kata  ya Kipunguni  kwa kazi nzuri wanazozifanya hivyo amewaomba wajasiriamali  waliopata mkopo waweze kurudisha kwa wakati ili kuwapatia fursa wajasiriamali wengine kupata mkopo na kuendesha biashara zao.

Akitoa taarifa fupi ya vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Afisa maendeleo wa Kata ya Kipunguni Bi. Rozina Soka ameeleza kuwa Kata ya Kipunguni ni miongoni mwa Kata 36 za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambazo zimenufaika na mikopo ya asilimia 10% za mapato ya ndani inayolenga kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuanzia mwaka 2019 hadi kufikia mwaka 2021.

Aidha Bi.Rozina  ameendelea kusema hadi kufikia Disemba 2021 Kata ya Kipunguni imeweza kusajili vikundi 46 ambavyo vimepokea mkopo wa shillingi milioni 432.5 ambapo vikundi  thelathink (30)  vya wanawake wamepokea shilingi milioni 217 huku vikundi kumi na nne (14) vya vijana vimepokea shilingi milioni 159.5 na vikundi viwili  (2) vya watu wenye ulemavu vimepokea jumla ya shilingi milioni 56. 

Sambamba na hilo Bi Rozina Soka amesema " Tunaishukuru Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya maendeleo ya jamii kwa kutuwezesha kupata mikopo japo kuna changamoto katika ufuatiliaji wa marejesho lakini sisi kama  viongozi tumeandaa mikakati ya ufuatiliaji  ngazi ya kata lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zote za mkopo zinarejeshwa kwa wakati na vikundi vingine vinavyoomba mikopo viweze kupatiwa kwa wakati.

Vilevile shillingi milioni 598 inatarajiwa kutolewa kwa vikundi takribani arobaini na moja(41) ambavyo vishajadiliwa kwenye kikao cha kamati ya fedha na mara tu watakapokamilisha  taratibu zilizobaki watapatiwa mkopo huo.

Akitoa wito kwa wananchi   kwa niaba ya wajasiriamali wenzake wa Kata ya Kipunguni Bi. Mboni  Edd Gamuya amesema "Napenda kumshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuona tija ya kutupatia mkopo  kwani mikopo hii imeweza kutukwamua kiuchumi na pia kwa kiasi kikubwa imeweza kutatua tatizo la ajira kwa vijana wengi.Pia ningependa kutoa wito kwawajasiriamali wenzangu ambao wanasuasua kurejesha mikopo yao warejeshe kwa wakati ili kuwapatia fursa wananchi wengine wanaoomba mikopo waweze kupata mikopo kwa wakati na kuweza kuendesha biashara zao.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.