Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Ng'wibuzu Ludigija leo tarehe 4 Oktoba 2022 amefanya ziara ya kukakuga miradi ya kimkakati ya ujenzi wa kituo cha afya Kipunguni B, jengo la huduma za dharura Zahanati ya Magereza Ukonga na Hosptali ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kivule, katika ziara hiyo ilijumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ilala, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala sambamba na Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo ya kamati ya ulinzi na usalama ya Jji la Dar es salaam imetembelea na kukagua maendeleo ujenzi kituo cha afya cha kipunguni B ambacho kinajengwa wa fedha za tozo kutoka Serikali Kuu, ujenzi wa jengo la dharura katika hospitali kuu ya Magereza Ukonga pamoja na jengo la huduma za bima na binafsi kwenye hospitali ya Wilaya - Kivule
Akikagua maendeleo ya ujenzi katika maeneo hayo Mkuu wa wilaya ya Ilala amemuagiza kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dar ea salaam Mhe. Eng. Amani Mafuru,Kusitisha na kuvunja mikataba wa mkandarasi SUMAJKT na mshauri elekezi TBA anayejenga jengo la huduma za bima na binafsi katika hoapital ya wilaya kivule.amesema "Nasikitika taasisi za serikali SUMA JKT sambamba na TBA kushindwa kusimamia na kufanya kazi hii kwa ufanisi na kuendana na wakati,sababu zinazotolewa hapa hazifurahishi kutokana na hali hii maelekezo yangu kwako Mkurugenzi ili kunusuru mradi huu ni kuvunja mkataba".
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo lililopo katika hosptali ya kivule ni muhimu sana kwani pindi mradi huu ukikamilika kwa wakati utasaidia na kutoa huduma kwa wananchi kutoka kata zote katika Halmashauri ya jiji la Dar es salaam akiongeza Mkuu wa Wilaya katika hilo amesema malengo ya Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wananchi wapate Huduma.
Hata hivyo maendeleo ya miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbaki isipokuwa kwenye baadhi ya maeneo Ludigija amewataka wakandarasi kuongeza kasi ili miradi ikamilike kwa wakati kwani ukamilifu wa Miradi hiyo itakuwa chachu ya huduma bora kwa wananchi. "ujenzi wowote katika miradi hii tunahitaji kuona thamani ya fedha inayotolewa na serikali iendane na jengo husika kuchelewa kwa kukamilika mradi kunasababisha hasara na matumizi mabaya ya fedha" amesema Mheshimiwa Ludigija
Akihitimisha ziara hiyo Mheahimiwa Ludigija ametoa wito kwa watekelezaji wa miradi pamoja na wasimazi kutoka Halmashauri kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa ukaribu zaidi kwani hii itasaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa weledi zaidi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.