Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita Charles na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 27 Aprili, 2018 wamefanya ziara katika visiwa vya Mbudya na Bongoyo vilivyopo katika bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam na kujionea fursa mbalimbali za kitalii ndani ya visiwa hivyo.
Akiongea mbele ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari katika ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tayari ilishazindua mpango wa kukuza na kuendeleza utalii jijini Dar es Salaam na kinachofanyika hivi sasa ni kutoa hamasa kwa wakazi mbalimbali wa Jiji na wageni kutoka ndani na nje ya nchi kuweza kuvitembelea vivutio vya utalii katika Jiji la Dar es Salaam.
Awali akiwasilisha taarifa ya uhifadhi ya maeneo tengefu ya utalii jijini Dar es Salaam kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Afisa Mfawidhi wa Maeneo Tengefu jijini Dar es Salaam, Bi. Anitha Julius Kilewo ameeleza kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii katika visiwa vya Mbudya na Bongoyo ikiwemo miti ya asili ya Mivinje, Kaa anayepanda mti, Kaburi la Sultani lenye zaidi ya miaka 200, Matumbawe, maji masafi na mchanga mzuri, Boma la kihistroria la Wajerumani "Germany house" lililojengwa miaka ya 1850's, samaki wazuri, Komboo "Dolphin" na makazi ya ndege wanaohama kutoka bara la Ulaya kipindi cha baridi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.